MKUU wa chama cha kihafidhina nchini Austria cha People’s Party, Sebastian Kurz, anaelekea kupata ushindi wa kuliongoza taifa hilo akiwa na umri mdogo, anaandika Hamis Mguta.
Kurz mwenye umri wa miaka 31 yupo katika nafasi nzuri ya kuunda serikali ya muungano.
Haijulikani wazi iwapo atafikiria kuunda serikali ya muungano na chama kinachopinga uhamiaji Freedom Party, kilichoibuka nafasi ya tatu katika uchaguzi huo.
Akihutubia wafuasi wake, Kurz amesema “Ni wakati wa kuleta mabadiliko katika nchi hii, leo ni siku muhimu kwetu kuibadilisha nchi hii na ninasema asante kwa wale waliowezesha hili”.
Kabla ya uchaguzi, Kurz alishika nafasi ya Waziri akiwa na umri mdogo, akitumia nafasi ya Waziri wa Mambo ya Kigeni barani Ulaya wakati huo akiwa na miaka 27.
Mwezi Mei mwaka 2017 akawa kiongozi wa chama cha People’s Party.
Leave a comment