Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Kigwangalla aomba suruhu kwa MO Dewji
Michezo

Kigwangalla aomba suruhu kwa MO Dewji

Spread the love

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye Serikali ya awamu ya Tano, Dk. Hamis Kigwangallah ameomba kumaliza tofauti zake na mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji ‘MO’ mara baada ya wawili hao kuingia kwenye marumbano katika siku za hivi karibuni kuhusiana na uwezekezaji wa Bilioni 20 katika klabu ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kigwangallah ametoa taarifa yake ya kuomba suruhu hii leo kupitia ukurasa wake rasmi kwenye mtandao wa kijamii instagram huku akiomba radhi kwa mfanyabiashara huyo na mashabiki wa Simba aliowakwaza na kueleza kuwa yeye amesamehe.

Sintofahamu kati ya Waziri huyo mstaafu na Mo Dewji ilikuja mara baada ya Kigwangalla ambaye pia ni mwanachama wa klabu hiyo kutilia shaka uteuzi wa mtendaji mkuu wa sasa wa Simba, Barbara Gonzalenz kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter na kuandika kuwa kilichofanyika kwenye uteuzi huo ni ujanja ujanja.

Aidha Kigwangallah aliendelea kwa kuandika kuwa mabadiliko yaliyompa Mo Dewji kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ndani ya Simba hayajakamilika kwa kuwa hajalipa Sh. 20 bilioni, na yeye kushangaa kwa nini anafanya uteuzi huo.

Mara baada ya kuandika hivyo, muda mfupi uliofuata Mo Dewji aliandika kwa kumjibu juu ya mjadala huo kwa kusema kuwa si kitu vizuri kuomba mtu yoyote apigwe mawe na kueleza kuwa swala la uwekezaji wake ameshalizungumza kwenye vyombo vya Habari na alifika mbali na kueleza kuwa angeweza kumpigia simu kwa kuwa namba yake anayo.

“Mhe.Kigwangalla, sio utu kumuombea mtu yoyote apigwe mawe. Suala la uwekezaji Simba nililielezea kwenye interview na Wasafi FM. Wengi wameelewa. Itafute. Kama bado hutaelewa, namba yangu unayo nipigie nitakufafanulia. Pia nisamehe kwamba mkopo wa pikipiki ulioniomba haikuwezekana,” aliandika mfanyabiashara huyo.

Mara baada ya maneno hayo, mjadala huo ulihama na kuanza kujadiliwa swala la Waziri huyo kunyimwa mkopo wa pikipiki na kuhisi pengine swala hilo ndio lililopelekea kumvaa mwekezaji huyo wa Simba.

Katika taarifa yake aliyoitoa hii leo Kigwangallah alieleza ni kwa namna gani alivyokutana na mfanyabiashara huyo na mpaka kufikia hatua ya kutaka kukopa pikipiki ili aweze kuendesha biashara zake na pesa hizo angeweza kurudisha ndani ya mwezi mmoja.

Kikao cha Bodi ya Simba

Kigwangallah ameendeloea kueleza kuwa Mo Dewji hakupaswa kutoa siri za biashara zao hadharani jambo ambalo anaamini kuwa lililenga kumdhalilisha na kumchafua.

Mchakato wa uwekezaji ndani ya Simba hivi sasa unapitia changamoto nyingi kiasi cha wadaua wengi kutaka kujua umefikia wapi, licha ya hivi karibuni mwekezaji huyo kusema kuwa mchakato huo upo kwenye mikono ya Tume ya Ushindani Kibiashara (FCC) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari tarehe 15 Novemba, 2020.

Mara baada ya kauli hiyo tulishuhudia FCC waliibuka na kusema kuwa kukwama kwa mchakato huo unasababishwa na uongozi wa Simba wenyewe kwa kushindwa kuwasilisha baadhi ya nyaraka mbele ya tume hiyo kwa ajili ya uchunguzi.

Ikumbukwe tarehe 3 Decemba, 2017, mfanyabiashara Mo Dewji alishinda zabuni ndani ya klabu hiyo kwa kupata hisa asilimia 49, kwa kiasi cha Sh. 20 bilioni, katika mchakato uliondeshwa na kamati maalumu ya mabadiliko ya klabu hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Mihayo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!