Wakili Simon Patrick

Kigogo Yanga asimamishwa kazi

Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga imemsimamisha kazi Kaimu Katibu Kkuu wa klabu hiyo, Wakili Simon Patrick ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa sheria na wanachama ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ambazo hazikuwekwa wazi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya kamati hiyo kufanya kikao cha dharura kilichofanyika tarehe 17 novemba 2020, kwa ajili ya kujadili swala hilo.

Katika taarifa yao ambayo imesainia na Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla imeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo, ili kuhakikisha haki inatendeka kamati ya utendaji itateuwa kamati huru kuchunguza jambo hili na kutoa maamuzi yenye tija kwa pande zote.

Wakili Simon amekaimu nafasi hiyo ya katibu mkuu mara baada kuondolewa kwa aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo Dk. David Luhago tarehe 16 Juni, 2020.

Kwa maamuzi hayo, Wakili Simon atakuwa katibu mkuu wa pili kuhudumu katika nafasi hiyo toka Msolla alipoingia kwenye madaraka ndani ya klabu hiyo.

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga imemsimamisha kazi Kaimu Katibu Kkuu wa klabu hiyo, Wakili Simon Patrick ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa sheria na wanachama ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ambazo hazikuwekwa wazi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea). Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya kamati hiyo kufanya kikao cha dharura kilichofanyika tarehe 17 novemba 2020, kwa ajili ya kujadili swala hilo. Katika taarifa yao ambayo imesainia na Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla imeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo, ili kuhakikisha haki inatendeka kamati ya utendaji itateuwa kamati huru kuchunguza jambo hili na kutoa maamuzi yenye…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!