Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kigamboni, Mkuranga watangaziwa neema ya maji
Habari Mchanganyiko

Kigamboni, Mkuranga watangaziwa neema ya maji

Bomba la maji
Spread the love

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), Jenerali Davis Mwamunyage amesema, tatizo la maji kwa wakazi wa Kigamboni na Mkuranga litamalizika kuanzia Aprili 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwamunyange ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi mstaafu, amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na Dawasa katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam na Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Amesema, anatambua hitaji la maji kwa wananchi wa maeneo hayo hivyo, mamlaka anayoisimamia inakwenda kumaliza changamoto hiyo kwa haraka ili huduma ya maji ibaki kuwa historia.

Mwamunyange amesema, kwa sasa ujenzi wa miradi hiyo inaendelea katika hatua nzuri, wakandarasi wanaendelea kwa kasi ambapo hadi kufikia Aprili 2021 hitajio la maji kwa wananchi hao litafika mwisho.

“Mradi huu wa visima vya Kimbiji na Mpera ni moja ya mradi mkubwa sana, utamaliza tatizo la maji kwa eneo la Mkuranga na Kigamboni na baadhi ya maeneo ya Temeke” amesema Mwamunyange

DAWASA inatekeleza mradi wa Maji katika Wilaya ya Mkuranga unaogharimu kiasi cha Sh. 5.5 bilioni na utahudumia wakazi takribani 25,000 huku wilaya ya Kigamboni inatekeleza mradi mkubwa wa Sh. 8.7 bilioni utakaohudumia wakazi 450,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!