Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kifo cha Rais Nkurunzinza, Majaliwa asaini kitabu cha maombolezi
Habari Mchanganyiko

Kifo cha Rais Nkurunzinza, Majaliwa asaini kitabu cha maombolezi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kwenye Ubalozi wa Burundi, Upanga, Dar es salaam, Juni 17, 2020. Wa pili kulia ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Abayeho Gerva
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza na kutoa pole kwa wananchi wa nchi hiyo kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli.

“Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, nimekuja hapa kutoa pole na salamu za rambirambi kwa Serikali na wananchi wa Burundi kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi ya Burundi. Mheshimiwa Rais na Watanzania wote tumepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa za kifo chake,” amesema

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 17 Juni  2020 akiwa katika Ofisi za Ubalozi wa Burundi, Upanga jijini Dar es Salaam baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Nkurunziza aliyefariki tarehe 9 Juni 2020 kutokana na mshituko wa moyo.

Amesema Tanzania na Burundi ni nchi zenye historia ndefu na mshikamano wa muda mrefu, hivyo ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wa Burundi wawe watulivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kwenye Ubalozi wa Burundi, Upanga, Dar es salaam, Wa pili kulia ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Abayeho Gervais.

“Serikali ya Tanzania itaendelea kudumisha umoja na mshikamano kati yake na Burundi,” amesema

Awali, Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Balozi Abayeho Gervais ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa kwa Taifa hilo na kwamba anatarajia umoja na mshikano huo utadumu milele na milele.

“Tunamshukuru Rais wa Tanzania amepeleka ujumbe mkubwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais mstaafu waJakaya Mrisho Kikwete nchini Burundi kwa ajili ya kushuhudia uapishwaji wa Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye anatarajiwa kuapishwa kesho Juni 18,” amesema

Akizungumzia kuhusu kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Balozi Gervais amesema, wamepokea kwa mshtuko mkubwa kwa sababu alikuwa bado ni kijana akiendelea kufanya shughuli zake. “Hii yote ni mipango ya Mwenyezi Mungu na sote tupo safarini.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!