Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kifo cha Rais Nkurunzinza, Magufuli atangaza maombolezo siku tatu
Habari Mchanganyiko

Kifo cha Rais Nkurunzinza, Magufuli atangaza maombolezo siku tatu

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli ametangaza maombolezo ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia leo Jumamosi tarehe 13 hadi 15 Juni, 2020 kufuatia kifo cha Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Nkurunzinza alifariki Jumanne tarehe 9 Juni 2020 kwa mshtuko wa moyo.

Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa usiku tarehe 12 Juni 2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza, katika kipindi chote cha siku tatu za maombolezo ya Kitaifa, bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti.

Rais Magufuli ameeleza, Tanzania inatoa heshima hiyo kwa kifo cha Pierre Nkurunziza kwa kutambua alikuwa Rais wa nchi jirani ambayo imekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri, wa kirafiki, kihistoria na kidugu na Tanzania.

“Burundi ni mwanachama mwenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mhe. Rais Nkurunziza aliipenda Jumuiya hii.”

Rais John Magufuli

“Pia, aliipenda Tanzania na alishirikiana nasi kila ilipohitajika, hivyo nimeona Watanzania tuungane na ndugu zetu wa Burundi katika kuomboleza na kumkumbuka Rais Nkurunziza ambaye aliiona Tanzania kama nyumbani kwake” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amerudia kutoa pole kwa Mama Denise Bucumi, Mjane wa Rais Nkurunziza, familia, Serikali na Wananchi wote wa Burundi kwa kuondokewa na mpendwa wao na amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!