Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kifo cha Mkapa, Chadema yaahirisha mikutano kuwapata wagombea urais
Habari za Siasa

Kifo cha Mkapa, Chadema yaahirisha mikutano kuwapata wagombea urais

Spread the love

CHAMA Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, Chadema kimetangaza kuahirisha mikutano yake iliyokuwa ianze tarehe 27 hadi 29 Julai 2020 ili kupisha maombolezo ya kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa nchi hiyo, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkapa alifikwa na mauti usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya Hospitali jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wake, utaanza kuagwa kesho Jumapili tarehe 26 hadi 28 Julai 2020 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kisha utasafirishwa kwenda kijijini Lupasa, Masasi Mkoa wa Mtwara Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020 makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Benson Kigaila amesema, mikutano hiyo imesogezwa mbele ili kutoa fursa ya Watanzania kuomboleza kifo cha Rais mstaafu Mkapa.

Akitangaza mabadiliko ya ratiba, Kigaila amesema, kikao cha kamati kuu kilikuwa kikutane tarehe 27 Julai 2020 sasa kitafanyika Agosti 2, 2020. Baraza Kuu tarehe 28 Julai 2020, kimesogezwa mbele hadi Agosti 3, 2020 na mkutano mkuu uliokuwa ufanyike tarehe 29 Julai 2020 sasa utafanyika tarehe 4 Agosti 2020.

Amesema, mikutano hiyo yote itafanyikia ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali hususan kuwapata wagombea urais wa Tanzania na Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali. Pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!