Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kibatala apinga Sinema ya Mbowe kuoneshwa Mahakamani
Habari za SiasaTangulizi

Kibatala apinga Sinema ya Mbowe kuoneshwa Mahakamani

Spread the love

UPANDE wa utetezi kwenye kesi namba 112 ya uchochezi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umepinga kuoneshwa kwa video iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Video hiyo ipo kwenye kielelezo namba 5 Mid-Div (tepu za kurekodia) na kile namba tano kamera iliyodaiwa mahakamani hapo kurekodiwa na Shahidi namba 6 (Kolpo Charles ambaye ni mpiga picha wa wa jeshi la Polisi).

Katika kesi hiyo watuhumiwa ni pamoja na Freeman Mbowe, Mwenyeki wa (Chadema)-Taifa, Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu (Chadema)-Taifa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo uliwakilishwa na Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, Wakili wa Serikali Mkuu na Wankyo Simoni Wakili wa Serikali Mwandamizi.

Huku upande wa utetezi umeongozwa na Profesa Abdallah Safari akisaidiwa na Peter Kibatala, John Mallya na Hakimu Mwasipu.

Leo tarehe 26 Julai mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, upande wa mashtaka umeomba kamera kuwa kielelezo namba nne na namba tano.

Wakili Kadushi: Kielelezo namba nne ni kielelezo gani?

Shahidi: Video kamera.

Wakili Kadushi: Hivi vielelezo namba 5 ni kitu gani?

Shahidi: Min-Div.

Wakili Kadushi: Wakati unaopiga picha za video hizi Min-Div zinakuwa wapi.

Shahidi: Ndani ya kamera.

Wakili Kadushi: Kwa muktadha huo unapopiga picha za video kumbukumbu zinahifadhiwa wapi kati ya kielelezo namba nne na namba tano.

Shahidi: Namba tano Min-Div.

Wakili Kadushi: Sasa shahidi wakati unatoa ushahidi uliiambia mahakama kuna namna mbili ya kutazama picha kwenye hii kamera na ukasema kwa namna ya kwanza unacheza video kupitia kamera yenyewe kupitia kitu gani?

Shahidi: LCD.

Wakili Kadushi: Lakini umesema kuwa kifaa kingine kinaweza kuonesha picha sauti ikiwa kubwa na sauti ikiwa kubwa ni sahihi?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Kadushi: Uliambia mahakama hii kitendo cha kuitazama video kutoka kwenye kamera hii kwa chanzo cha pembeni hakiathiri kwa namna yoyote ya uhalisia wa video hiyo?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Kadushi: Kwa namna gani mahakama inaweza kuangali video hizo?

Shahidi: Kutoka kwenye kamera kwenda kwenye screen au Projector kupita nyaya ya HDMI.

Wakili Kadushi: Kwa mujibu wa maelezo ya shahidi namna ambayo ametoa ushahidi wake mahakama inaweza kuangalia ushahidi kupitia screen kupitia nyaya ya HDMI tunaiomba Mahakama hii njia wezeshi ili kumbukumbu za ushahidi zilizokuwepo kwenye kielelezo namba tano zionekane kwa maana ya kisheria.

Kadushi ameendelea kuisitiza mahakama kupata mazingira wezeshi kwa ajili ya mahakama kuiona video.

Kibatala amedai kuwa utaratibu wa kuionesha mahakama ushahidi huo ni wajibu wa upande huo uandae mazingira aidha kwa kuimbia mahakama ihamie kwenye mazingira wezeshi au wenyewe kuja na Projecta kwa ajili ya kuonesha video.

Ameeleza kuwa hata hizo nyanya za kuonyesha video hizo hazijatajwa kwenye ushahidi.

Ameitaja kesi ya Mafie na wenzake ili kwenye mahakama ya biashara kwamba Jaji aliyesikiliza kesi hiyo aliutaka upande uliotaka kutoa ushahidi mahakamani hapo wafanye maandalize ya mazingira wenyewe. “Ni sawsawa na mtu aje na flash disk mahakamani aiombe laptop mahakama.”

Amesisitiza hata chaji ya kamera hiyo lazima isitoke nje lazima iwe imetaja kwenye ushahidi.” Kwa hiyo sisi hata wangeomba waya ya kuchajia mahakamani tungepinga … kwa sababu hayo hayajafanyika tunaomba kielelezo namba nne na namba vichukuliwe kama vilivyo.

“Tunapinga chochote kufanyika kwa vielelezo hivyo vinginevyo shahidi aendelee kuelezea maelezo ya vielelezo hivyo,” alisema Kibatala.

Wakili Kadushi ameeleza kuwa umesikia hoja za upande wa utetezi na kwamba hoja zote mbili zilizotolewa na Kibatala sio hoja za kisheria zinazokidhi matakwa ya kisheria.

“Ili pingamizi liwe pingamizi kisheria ni lazima lianishe kifungo cha sheria au sheria fulani itakayoielekeza mahakama … yote aliyoyaongea ni maoni binafsi,” ameeleza Kadushi.

Amedai kuwa hatua aliyoieleza Kibataka washaipita na kwamba vielelezo vishapokelewa pia hoja ya kuwa watapinga hata wakileta waya wa chaji sio kile kinachotolewa mahakamani ni lazima kiwe ushahidi na alichosema kwamba tungeomba ukumbi wa mikutani huo sio utaratibu wa kisheria hoja hiyo inakinzana na hoja yake mwenyewe ya kwamba mazingira tuyaandae wenyewe wakati huo huo anasema tungeomba ukumbi wa mikutano ambao upo chini ya idara ya Mahakama.

“Ni rai yetu kwamba hoja ya kwamba tungeomba jengo la utawala sio jukumu letu na miundombinu yote inapaswa kuwa chini ya mahakama wenyewe ni jukumu la mahakama kuandaa mazingira ya kusikiliza ushahidi kwa muktadha huo tunarejea ombi letu Mahakama iwezeshe vielelezo visomwe au vioneshe,” amedai Kadushi.

Amedai kwa vile nyanya au chaji sio kitu muhimu kwenye kupokelewa ushahidi huo.

Kibatala amedai kupeleka maombi mahakamani ni maombi ya kimahakama na sio maombi ya kiutawala na kwamba maombi ya kiutawala yanautaratibu wake.

Amedai kuwa shahidi aliieleza mahakama kuwa ili hiyi video ionekane kwenye screen lazima awe na nyaya ameiita (fire), ambayo haikutajwa mahakamani kama ilivyoelezwa kielelezo cha tano.

Profesa Safari ameeleza mahakamani hapo kwa mfano ingekuwa kesi ya madai ilhali mahakama imetoa mazingira ya ushahidi tungesema mahakama imependelea.

Baada ya mabishano makali ya kisheria ya pande zote mbili Hakimu Simba ameihalisha kesi hiyo na kusema kwamba kesi hiyo inatakiwa iendeshwe haraka kwani sasa ishafika mwaka na nusu kwani imeenza Mwezi Machi Mwaka 2018 hivyo anataka kuendelea kusikiliza mfulilizo.

Hakimu Simba ameahilisha kesi hiyo mpaka terehe 5,6 na 7 mwezi Agosti kwa ajili ya kutoa uamuzi juu ya kutazama video iliyorekodiwa na Koplo Charles.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!