Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kibano: Shahidi Serikali Vs Mawakili wa Mbowe, wenzake
Habari za SiasaTangulizi

Kibano: Shahidi Serikali Vs Mawakili wa Mbowe, wenzake

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inaendele na usikilizwaji wa kesi namba 112, ya mwaka 2018, inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kwenye kesi hiyo watuhumiwa ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa; Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Bara; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Zanzibar; Ester Matiko, Mhadhini wa Baraza la Wanawake la Chadema-Taifa.

Wengine ni Peter Msigwa, Mbunge Iringa Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini.

Tarehe 13 Mei 2019 mawakili wa utetezi waliongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya, Hekima Mwasipu na John Mallya.

Mtandao huu unakuletea mahojiano maalum kati ya shahidi na upande wa utetezi kama ifuatavyo;-

Mtobesya: Hebu isaidie mahakama kwa ajili ya uelewe, mnavyoingia kazini mnaweka sehemu gani kumbukumbu kuwa mmeingia kazini?

Shahidi: Kwenye Kitabu

Mtobesya: Kinaitwaje?

Shahidi: Kitabu cha mahudhurio

Mtobesya: Wakati unaongozwa na wakili Nchimbi hakupata wasaa wa kutoa hiko kitabu kuonesha kuwa tarehe 16 Februari ulikuwa kazini?

Shahidi: Sikutoa.

Mtobesya: Ulisema gari iliyokuwa unatoa Ilani na waandamanaji uliowataja kuwa kina Salum Mwalimu, ulisema ni kama mita 100?

Shahidi: Sikusema mita mia.

Nilisema nilianza kutoa Ilani nilipokuwa karibu yao na nilipowapita nikatoa Ilani nilikuwa mita 100. 

Mtobesya: Kwa uhakika  ilikuwa muda gani?

Ulisema ni saa 11 kwenda 12 ?

Shahidi: Saa 11 kwenda 12 jioni

Mtobesya: Kwa ushahidi wako, mita 100 unaweza kuona kinachoendelea muda huo?

Shahidi: Ndio.

Mtobesya: Unaujua umbali wa mita mia?

Shahidi: Ndio. Kama uwanja mmoja wa mpira.

Mtobesya: Kwa hapa tulipo kadiria?

Shahidi: Hapa hadi (korti) getini.

Mtobesya: Kwenye ushahidi wako, ulisema kati ya hao watu 600 kutoka hapa hadi getini ungeweza kuwaona sawasawa kwa umbali wa hapa hadi getini?

Shahidi: Ndio

Mtobesya: Kwa utabiri wa hali ya hewa kwa siku hiyo Mawio kwa siku hiyo nitakuwa sahihi?

Shahidi: Nilichosema mimi muda wa saa 11 hadi 12 mwanga unakuwepo.

Mtobesya: Nitakuwa sahihi siku hiyo giza lilianza kuingia saa 12 na robo kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa?

Shahidi: Sijui kama utakuwa sahihi.

Mtobesya: Wakati unaongozwa Nchimbi ulisema, ile njia inatumika na watu muhimu wakiwamo wagonjwa hakuna wakati ambao njia ile husimamishwa kwa dakika 45 hadi 30 ili viongozi wa kiserikai wapiti?

Shahidi: Upo.

Mtobesya: Na ni barabara hiyo hiyo uliyosema kwenye maelezo yako?

Shahidi: Ndio.

Mtobesya: Hebu tusaidie wewe haukuwepo kwenye tukio.

Kwa uwelewa wako wewe kusanyiko lisilo halali ni maandamano?

Shahidi: Sio kweli.

Mtobesya: Mueleze hakimu kwamba, ni wakati gani kusanyiko lile lilikuwa sio halali?

Shahidi: Wakati walipotoka Buibui waliambizana kwenda kwenye Ofisi za Mkurugenzi ndio walipoanza maandamano hayo.

Mtobesya: Ulijuaje na hukuwepo eneo la tukio?

Shahidi: Tulikuwa tunawasiliana kwenye simu na mawasiliana mengine ya kipolisi.

Mtobesya: Ulitoa Print-out (chapisho) lolote mahakamani kuhusu mawasilianao yenu?

Shahidi: Sikutoa.

Mtobesya: Waandamanaji ulikutana nao wapi?

Shahidi: Eneo la Mkwaju.

Mtobesya: Kwa hiyo, kama hawa watu ulikutana nao ulijuaje kama wanakwenda hapo kutafuta usafiri kwenda kwao?

Shahidi: Nilisikia kutoka kwa askari wengine kuwa walikuwa wanakwenda Kwa Mkurugenzi.

Mtobesya: Unajuaje kama watu hawa walibadilisha mawazo ya kupanda gari za kwenda makwao?

Shahidi: Walipotoka kuna vituo vya daladala.

Mtobesya: Wewe unajua wanaishi wapi mpaka wapande popote daladala?

Shahidi: Sijui.

Mtobesya alimaliza maswali yake kwa shahidi na ikiwa zamu ya wakili Mwasipu.

Mwasipu: Ni sahihi kuwa, hukuwepo viwanja Buibui wakati kampeni?

Shahidi: Sawa

Mwasipu: Ni sahihi kuwa taarifa za yaliyojiri mkutano ilizitoa kwa mtu anayeitwa Dotto?

Shahidi: Ni sahihi.

Mwasipu: Ni kwamba, maandamano uliyashuhudia yaliyoka njia panda kuja Mkwajuni.

Shahidi: Mkwajuni ni sehemu nyengine.

Mwasipu: Ni sahihi kwamba, hukuwauliza washatakiwa walikuwa wakienda kwa mkurugenzi kufanya nini?

Shahidi: Niliwaamuru watawanyike.

Mwasipu: Ni sahihi kwamba, uliwatawanya waandamanaji na hadi sasa hivi hujui malengo ya washtakiwa kwenda kwa mkurugenzi?

Shahidi: Ni sahihi.

Mwasipu: Ni sahihi kwa hukuwasiliana na mkurugenzi tangu siku ya maandamano?

Shahidi: Huwa tunawasiliana.

Mwasipu: Ulishawahi kuzungumza na mkurugenzi juu ya maandamano hayo?

Shahidi: Sikuzungumza naye.

Mwasipu: Ni sahihi kwamba, baada ya mkutano kuisha watu wanatakiwa warudi nyumbani kwako hawatakiwi kubaki uwanjani?

Shahidi: Sahihi.

Mwasipu: Ni sahihi kwamba, hufahamu makazi ya watu waliokuja kwenye viwanja Buibui?

Shahidi: Ni sahihi.

Mwasipu: Ni sahihi pia kuwa, hujui nyumbani kwa washitakiwa?

Shahidi: Sifahamu

Mwasipu: Ni kosa au sio kosa waandamanaji wakiongoza zaidi ya mmoja?

Shahidi: Watatu, wane, watano sio kosa.

Mwasipu: Kinachoharamisha mkutano ni sababu au ni kusanyiko lisilohalali?

Shahidi: Vyote sababu na kusanyiko.

Mwasipu: Umeupata wapi uhalali wa kuwatanya waandamanaji?

Shahidi: Uhalali nimeupata baada ya wao kugeuza mkutano uliokuwa halali kuwa maandamano.

Mwasipu: Wakiongozana zaidi ya mmoja kwenda kwenye ofisi ya mkurugenzi kwenda kuchukua hati ya kiapo kwa mkurugenzi ni halali au sio halali?

Shahidi: Watu 10 halali.

Amemaliza Mwasipu amemkabidhi kijiti Profesa Safari 

Prof. Safari: SSP Ngichi ulipokuwa unahojiwa na Kibatala ulisema kuwa, Dotto ndiye aliyekupigia simu kukuambia kuwa viongozi wa Chadema wamendamana?

Shahidi: Ndio.

Prof. Safari: Ulisema kuwa, sababu ya kuwazuiya ni Ofisi za Serikali zilikuwa zimefungwa?

Shahidi: Ndio.

Prof Safari: Ulijuaje?

Shahidi: Kwa kawaida Saa tisa na nusu ofisi za serikali hufungwa.

Prof Safari: Huo ni wakati wa uchaguzi ofisi zina kuwa wazi?

Shahidi: Sio kweli.

Prof Safari: Wewe ni mwanasheria?

Shahidi: Ndio

Prof Safari: Ni kweli Katiba inamtaka mtu kwenda anapotaka.

Shahidi: Ndio.

Prof Safari: Unajua kuwa, tarehe 10 mwenzi huu Mahakama Kuu ilipiga marufuku wakurugenzi kuhusika uchaguzi kwa sababu wanakuwa na upendeleo?

Shahidi: Nilisikia kwenye vyombo habari.

Prof Safari: Ni sahihi kuwa, kuna watu mliwaweka kwenye vituo vya polisi wakiwa na majeraha?

Shahidi: Sio kweli.

Prof Safari: Kamanda Mambosasa aliongea na vyombo vya habari kuhusiana na tukio la kuawa kwa Akwelina?

Shahidi: Sikumbuki

Prof Safari: Umewahi kutoa maelezo popote kuhusiana na kesi kabla hujaja kutoa maelezo?

Shahidi: Ndio.

Prof Safari:Tunaweza kuyapata maelezo yako?

Shahidi: Sijui mwendesha mashtaka.

Mheshimiwa tunaomba tuletewe maelezo yake aliyoyatoa.

Prof Safari:Tunaomba tuletewe maelezo ya shahidi aliyoyatoa kabla ya kuja mahakamani.

Mabishano yaliibuka juu ya ombi la Prof. Safari la kutaka maelezo ya shahidi.

Hakimu Simba amesema kuwa, ataacha upande wa Jamhuri uendelee na kumpitisha shahidi wao juu ya maswali aliyoulizwa.

Lakini Kadushi alidai kuwa, suala hilo ni la kisheria na ni vema likabaki kwenye rekodi za mahakama na kuwa, kifungu hiko kinatumika kwenye mahakama kuu endapo shahidi anakuwa hana msimamo na majibu yake

Upande wa serikali ulimalizia kumpitisha shahidi wao kwenye masahihisho ya maswali aliyoulizwa,

Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi alimuuliza ifuatavyo;

Nchimbi: Wakati unahojiwa na Kibatala alikuhoji kuhusu majina Akwlin, katika mahojiano hayo ulimtaja Akwelin kwa jina moja tu ni kitu gani kilichokufanya mtaje kwa jina moja?

Shahidi: Mimi nikiwa kama mkuu wa operesheni nawajibika kuhakikisha usalama na amani, sikuwajibika kujua majina ya watu.

Nchimbi: Ulishiriki upelelezi wowote kwenye kesi hii?

Shahidi: Sikushiriki.

Nchimbi: Ulisema kuwa, hujui sababu za kifo cha Akwelina labda kwanini hujui?

Shahidi: Kwanza mimi sio daktari, siwezi kujua sababu za kifo cha mtu yoyote.

Nchimbi: Ulihusikaje na kuanda mashataka na upelelezi wa lesi hii?

Shahidi: Mimi sihusiki kwenye mashakataka, anayehusika ni mkuu wa upelelezi.

Nchimbi: Alikuuliza Kibatala kuhusu kuongea na watu wa Mkwajuni waliokuwa wakifanya biashara, na ulisema uliongea nao lakini hukueleza kwanini hukuchukua maelezo ya wafanyabiashara?

Shahidi: Mimi ni Mkuu wa Operesheni sikuhusika na masuala ya upelelezi.

Nchimbi: Ulisema watu hao ulizungumza nao ni jambo gani ulizungumza nao?

Shahidi: Kwasababu ya maandamano yale mimi na timu yangu tuliwafuata kuwatuliza na kuwaambia kuwa, wasiwe na hofu amani imerejea.

Nchimbi: Nini kinachokufanya usiwe na kumbukumbu ya wamiliki wa maduka wa maeneo ya pale Mkwajuni na watu uliongea nao?

Shahidi: Kwa sababu mimi nilikuwa kwenye operesheni ya kuzuia maandamano, kazi ya upelelezi niliwaachia wapelelezi.

Nchimbi: Kwanini unakosa kumbukumbu za kupotea kwa watoto na wazee?

Shahidi: Kumbukumbu hizo zinabaki kituoni na anayezihifadhi ni Mkuu wa Kituo.

Nchimbi: Kibatala alikupitisha kwenye hati ya mashataka kuanzisha shtika la kwanza, ulipata kuiona hati hiyo?

Shahidi: Sijaiona.

Nchimbi: Wewe ulihusika kwa namna gani kuiandaa hati hiyo ya mashtaka?

Shahidi: Mimi kama ofisa wa operesheni sihusiki na uandaji wa hati ya mashtaka.

Nchimbi: Wewe umekuja mahakamani kama nani?

Shahidi: Nimekuja kama shahada, nimekuja kutoa ushahidi.

Nchimbi: Umesema kuwa, hati ya mashtaka hujawahi kuiona wala kuianda, tusaidie maneno yale aliyokuwa akikuambia Kibatala yalitamkwa wapi?

Shahidi:Yalitamkwa kwenye kampeni za Chadema viwanja vya Buibui .

Nchimbi: Kibatala alikuuliza kuwa, huyu alivyotamka hivi huu alitamka vile, wewe ulikuwa wapi wakati maneno haya yanatamkwa?

Shahidi:Nilikuwa eneo jengine sikuwepo hapo.

Nchimbi: Kuna maswali hapa alihoji Kibatala kuhusiana na namna watuhumiwa walivyokamatwa . Tufahamishe watu hao walivyokamatwa ulishughulika nao vipi?

Shahidi: Mimi sikuhusika nao isipokuwa walikuwa chini ya Mkuu wa Upelelezi.

Nchimbi: Kitu gani kilikufanya kushindwa kuwakamata watuhumiwa hawa eneo la tukio?

Shahidi: Walikimbia.

Nchimbi: Jukumu lako la msingi kama ofisa wa operesheni ni lipi?

Shahidi: Jukumu langu ni kuzuia maandamano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!