Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi za ‘kimapinduzi’ kuanza kuunguruma
Habari Mchanganyiko

Kesi za ‘kimapinduzi’ kuanza kuunguruma

Spread the love

KESI za kupinga watuhumiwa kukamatwa kabla ya upelelezi kukamilika, pamoja na kunyimwa haki ya dhamana inaanza kutajwa leo tarehe 13 Februari 2020. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hizo zilizofunguliwa na Wanaharakati wa Haki za Binadamu nchini Tanzania, katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam.

Kesi ya kwanza Na. 35/2019, imefunguliwa na Paul Kisabo, Mwanasheria wa Mtandao wa Watetetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kupinga watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kunyimwa dhamana.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza leo tarehe 13 Februari 2020 mbele ya majaji watatu, Jaji  Dk.Benhajj Masoud, Jaji Magoiga na Jaji Juliana Masabo.

Kesi ya pili Na. 36/2019 imefunguliwa Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, inayopinga watuhumiwa wa makosa mbalimbai kufikishwa kwenye mahakama zisizokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi zao.

Pia, Olengurumwa anapinga watuhumiwa wa makosa mbalimbali kukamatwa bila ya upelelezi kukamilika.

Kesi hiyo pia inatarajiwa kutajwa leo mbele ya majaji watatu, Jaji Benhajj Masoud, Jaji Mlyambina na Jaji Juliana Masabo.

Katika kesi hiyo, Olengurumwa anaiomba mahakama hiyo kutoa tamko la kufuta vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20, kw amadai kwmaba vinakiuka haki na uhuru wa watuhumiwa, kuminya utawala wa sheria  pamoja na kufifisha mchakato wa uendeshaji kesi kwa usawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!