Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Zitto: Shahidi ‘niliona maiti watatu’
Habari za Siasa

Kesi ya Zitto: Shahidi ‘niliona maiti watatu’

Spread the love

SHAHIDI wa mwisho wa upande wa utetezi kwenye kesi namba 327/2018, inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameieleza mahakama kuwa aliona miili ya watatu watatu waliofariki porini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Shahidi huyu anayetimiza idadi ya mashahidi nane wa utete akiwemo na mshitakiwa mwenyewe (Zitto), ni Nasib Kakagila, Mkazi wa Kijiji cha Mpeta, Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza, Kigoma.

Shahidi huyo aliyeieleza mahakam kuwa, amefika mahakamani hapo kutoa ushahidi juu mapigano ya polisi na raia yaliyotokea Kijiji cha Mpeta, alijitambulisha mahakamani hapo kuwa ni mkulima wa mihogo, viazi na mahindi pia ni Katibu Chama cha ACT-Wazalendo, Tawi la Mpeta.

Leo tarehe 3 Aprili 2020, shahidi akiongozwa na wakili wa utetezi Jebra Kambole, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, ameeieleza mahakama kuwa tarehe 16 Oktoba 2018, askari wa Jeshi la Polisi walivamia kwenye Kijiji cha Mwanduhubandu.

Kwenye kijiji hicho, yeye anafanya shughuli zake za kilimo ambapo majira ya saa 11 alfajiri walianza kurusha risasi sambamba na mabomu ya machozi, huku wakichoma moto nyumba wakazi wa kijiji hicho.

Kakagila amedai kuwa wananchi kwa hofu kubwa walikimbia ambapo nyuma yao alisikikia sauti ya mwanakijiji akilalamika kwa lugha ya asili ya wakazi hapo kuwa “Ndugu zangu mimi nakufa”- amedai kuwa walikimbia kujificha kujinusuru.

Wakili Jebra: Wewe ulienda wapi?

Shahidi: Nilikimbilia porini.

Wakili Jebra: hiyo tarehe 16?

Shahidi: Ndio.

Wakili Jebra: Tarehe 18 ulishuhudia nini?

Shahidi: Tarehe 18 saa 3 kwenda saa asubuhi wananchi tukiwa tumekusanyika ghafla tukaanza kusikia milio ya risasi m askari waliturushia mabomu ya machozi mimi nilikimbia kurudi kijiji kabisa mpeta.

Wakili Jebra: Baada ya wewe kukimbia ulirudi tena?

Shahidi: Ndio nilirudi siku ya tarehe 19 Oktoba majira ya saa 10 jioni.

Wakili Jebra: Ulirudi kufanya nini?

Shahidi: Kuna dhana zangu za kilimo niliacha

Wakili Jebra: Dhana gani?

Shahidi: Majembe saba, mapanga matano, na mashoka matano.

Wakili Jebra: Ulishuhudia nini kama athari za mapigano?

Shahidi: Tarehe 19 sikupita njiani nikihofia nilipita njia za porini nilipokaribia shambani nilikuta miili ya watu watatu wamekufa.

Wakili Jebra: Ulifanikiwa kuchukua vifaa vyako?

Shahidi: Hapana nilishikwa na hofu nikakimbia kurudi kijijini Mpeta.

Wakili Jebra: Ulifanya nini?

Shahidi: Baada ya kurudi kijijini nitafakari cha kufanya nikaamua kuipeleka taarifa hiyo kwa viongozi wangu wa chama.

Wakili Jebra: Nani uliyempa taarifa hiyo?

Shahidi: Shabani Ali.

Wakili Jebra: Sasa hali ipoje?

Shahidi: Sasa hivi kuna utulivu.

Alipohojiwa na  Wakili wa Serikali Nassoro Katuga juu ya kwanini ametoa taarifa ya kiusalama kwa kiongozi wa chama ilhali serikali ipo, amejibu ameona polisi ndio waliofanya uvamizi huo hivyo hakuona sababu ya kwenda kutoa taarifa kwao.

Baada ya kuhojiwa na pande zote mbili upande wa utetezi umefunga pazia lake la ushahidi, umeiomba mahakama kupanga tarehe ya wao kuwasilisha hoja za majumuisho ili mahakama hiyo itoe hukumu, huku upande wa serikali hakuona haja ya kufanya hivyo.

Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi tarehe 28 Aprili 2020, kwa ajili ya mawasilisho ya hoja za mwisho na tarehe 29 Aprili 2020 kwa kulitaja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!