Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Zitto: Shahidi asema ‘nawachukia polisi’
Habari za Siasa

Kesi ya Zitto: Shahidi asema ‘nawachukia polisi’

Spread the love

SHAHIDI wapili kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, analichukia Jeshi la Polisi kutokana na matendo ya ukatatili kwa raia. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Leo tarehe 16 Mei2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi, upande wa serikali uliongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka, Nassoro Katuga na Wankyo Simon, umewaleta mashahidi wawili mahakamani hapo.

Upande wautetezi uliongozwa na Wakili Peter Kibatala, Jebra Kambole, Dickson Matata na Jeremiah Mtobesya.

Upande waserikali umemtambulisha shahidi wake mbele ya mahakama kuwa ni Mashaka Juma (29), Mkazi wa Kimara, Korogwe jijini Dar es Salaam.

Yafuatayo ni mahojiano ya Wakili Mkuu wa Serikali, Kweka na shahidi huyo:-

 Wakili Kweka: Shahidi ieleze mahakama unaishi wapi?

Shahidi: Kimara Korogwe

Wakili Kweka: Shughuli zako ni nini?

Shahidi: Msanii wafilamu,tamthilia.

Wakili Kweka: Ukisema nimsanii wa filamu na tamthilia unamaanisha nini?

Shahidi: Nina maanisha kuwa, hiyo ndio kazi yangu ina maana mimi ni msaani.

Wakili Kweka: Mahakama itawezaje kujua kuwa wewe ni masanii?

Shahidi: Ili itambue kuwa mimi ni msaani nishaigiza filamu nyingi kama ile ya Utata iliyokuwa ikioneshwa Channel Ten, Wazee Wapamba na Yakihese.

Wakili Kweka: Hii shughuli umeanza lini?

Shahidi: Takribani miaka 10 sasa hivi.

Wakili Kweka: Umeieleza mahakama hii kwamba unaishi Kimara Korogwe, upo hapo kwa muda gani?

Shahidi: Miaka miwili.

Wakili Kweka: Ieleze mahakama hii kuwa tarehe 29 Oktoba, 2018 ulikuwa wapi?

Shahidi:Nilikuwa Dar es Salaam.

Wakili Kweka: Tarehe 29 Oktoba unakumbuka kitu gani?

Shahidi: …Nikiwa Kimara Korogwe wakati nacheza drafiti, tulikuwa wengi alikuja mchezaji mwengine ambaye tunacheza naye kila siku anaitwa Frank Zongo, alipofika yeye akatuuliza.

Wakili Kweka: Akawauliza nani?

Shahidi: Anatuuliza sisi.Mnahabari yoyote?

Wakili Kweka:  Enhee

Shahidi: Tukamjibu,hatuna habari yoyote, akatuuliza habari ya jiji hamuijui?

Wakili Kweka: Enheee!

Shahidi: Tukamjibu kuwa sisi hapa habari ya jiji huyu nimemfunga mbili mimi kanifunga tatu.

Wakili Kweka: Endelea

Shahidi: Akasema mheshimiwa Zitto ndio habari ya jiji.

Wakili Kweka: Kwa maana gani?

Shahidi: Tulimuuliza kwa maana gani akasema subirini akatoa simu yake alivyotufungulia, tukakutana na habari ya Mheshimiwa Zitto Kabwe.

“Tulikaa kwa umakini, kaiweka tukawa tunaiangalia, tukamuona Mheshimiwa Zitto Kabwe akililaumu Jeshi la Polisi kwa mambo ya kadha wa kadha”.

Wakili Kweka: Enhee!

Shahidi: Alikuwa akizungumza kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likinyanyasa wananchi, linafanya mauji, linateka watu akiwepo Mheshimiwa Mo,Jeshi la Polisi limeenda kuwachukuwa watu Hospital kisha likawaua.

Wakili Kweka: Endelea.

Shahidi: Kwa kweli Mheshimiwa hakimu nilijiuliza mambo mengi sana.

Wakili Kweka: Alizungumzia watu waliochukuliwa hospital wamechukuliwaje?

Shahidi:  alisema kwa kutekwa.

Wakili Kweka: Wapi?

Shahidi: Kigoma Uvinza.

Wakili Kweka: Kitu kingine?

Shahidi: Amesema Mkuu wa Polisi Sirro ameshindwa kuwadhibiti Askari wake.

Wakili Kweka: Umemzungumzia Zitto Kabwe ni nani hasa?

Shahidi: Ni kiongozi wa Chama cha siasa ACT-Wazalendo.

Wakili Kweka: Wewe binafsi unamfahamu Zitto Kabwe?

Shahidi: Namfahamu.

Wakili Kweka: Unamfahamu kivipi na kuanzia lini?

Shahidi: Nimemfahamu zamani sana, tangu akiwa Chadema na nadhani miongoni mwa wafuasi wake nami nipo.

Wakili Kweka: Ukiaangalia hapa Mahakamani Zitto Kabwe yupo hapa?

Shahidi: Eee yupo hapa.

Wakili Kweka: Yupo wapi?

Shahidi: Yule pale (amenesha kidole kizimbani alipo mtuhumiwa).

Wakili Kweka: Hizi taarifa ulizichukuliaje?

Shahidi: Mimi nilizichukulia kwa mtazamo tofauti.

Wakili Kweka: Kivipi?

Shahidi: Kwa sababu akiongea kiongozi ambaye mimi namfuatilia sana, nililitoa thamani Jeshi la Polisi kama wanashindwa kulinda raia na mali zake basi hakuna haja ya kuwa na Jeshi la Polisi.

Wakili Kweka: Umeelezamlikuwa wengi pale kwenye drafiti wale wengine wamechukuliaje?

Wakili Kibatala: Anamtaka shahidi aeleze maoni yake.

Wakili Kweka: Naondoa swali.

Wakili Kweka: Watu mliokuwa pale mliichukuliaje hiyo taarifa?

Shahidi: Asilimia kubwa ya watu waliokuwa pale walichukua Jeshi la Polisi.

Wakili Kweka: Kwanini?

Shahidi: Kama leo Jeshi la Polisi linaua Kigoma kesho watauwa Dar.

Wakili Kweka: Baada ya kuangalia hiyo video nini ulikuwa muitikio wenu?

Shahidi: Wengi tulimpongeza Zitto Kabwe kwa ujasiri na ukakamavu wake na mpaka sasa hivi nalichukia Jeshi la Polisi.

Hakimu Simba: Ulichukia hadi sasa hivi?

Shahidi: Hadi sasa hivi siliamini Jeshi la Polisi labda Zitto Kabwe aje aniambie sasa lipo sawa.

Wakili Kweka: Baada ya hapo?

Shahidi: Mimi nilipaniki sana, kuna mchezaji mmoja  mtu mzima alikuja akanivuta pembeni na kuniuliza kwanini umepaniki, nikamwambia kama kiongizi wa polisi anashindwa kudhibiti mauaji nitaachaje kulichukia jeshi hilo.

Wakili Kweka: Enhee.

Shahidi: Baadaye aliniomba namba ya simu na nikajua tutawasiliana kama walivyo watu wengine.

Wakili Kweka: Baada ya hapo?

Shahidi: Nilipigiwa simu tarehe 30 Oktoba 2018, aliniomba nifike Osterbay.

Wakili Kweka: Nani?

Shahidi: Alijitambulisha kuwa yule niliyecheza naye drafiti na kuniomba nifike Osterbay.

Wakili Kweka:  Baada ya kukuambia hivyo?

Shahidi: Nilitii wito huo tarehe 31 nilifika Osterbay Polisi pale nikafanya mahojiano.

Niliongea kile nilichoongea, nilililaumu sanaJeshi la Polisi kwa kile walichofanya kwa mauaji, utekeaji wa watu na kushindwa kusimamia haki za raia na mali zao.

Wakili Kweka: Ulieleza kwanza uliona nini kwenye simu labda nini kilichokufanya ujue huyu ni Zitto Kabwe?

Shahidi: Namfahamu hata sauti yake nikiisikia najua huyu ni zitto kabwe.

Wakili Kweka: Alikuwa akiongea katika mazingira gani?

Shahidi: Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kulikuwa na vipasa sauti vingi aliingia pale akashangiliwa alileta utani kidogo kisha akafunguka hayo.

Wakili Kweka: Hiyo video ukiiona utaweza kuitambua?

Shahidi: Naitambua.

Wakili Kweka: Utaitambuaje?

Shahidi: Yale aliyoyaongea siku ile na siku alivaa ‘Kaunda Suti’.

Wakili wa Kweka amemaliza kumuongoza shahidi itaendelea Wakili wa Utetezi Peter Kibatala akimuuliza maswali Shahidi.

Itaendelea…

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!