Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya viongozi, wanachama 26 Chadema yakwama
Habari za Siasa

Kesi ya viongozi, wanachama 26 Chadema yakwama

Spread the love

KESI ya viongozi na wafuasi 26 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaokabiliwa na mashtaka saba yakiwamo kutoa lugha ya maudhi na kuharibu gari ya Magereza, imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa awali. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (eendelea).

Leo Ijumaa tarehe 28 Julai 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Thomas Simba shauri hilo lilapangwa kuanza uskilizwaji wa awali.

Wakili wa Serikali, Faraja Nguka ameiomba Mahakama hiyo kumpa muda wa kulipitia jalada la kesi hiyo kwa kuwa yeye amekabidhiwa leo Jumanne jalada hilo.

“Naiomba Mahakakama hii ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusoma hoja za awali Kwa kuwa leo hii nimekabidhiwa jalada la kesi hii hivyo naomba nilipitie,” amedai Faraja

Washtakiwa hao wakiwemo wabunge watatu wa chama hicho, Halima Mdee wa Kawe, Ester Bulaya wa Bunda Mjini pamoja na Jesca Kishoa wa Viti Maalum.

Wengine ni aliyekuwa meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, aliyekuwa Diwani wa Tabata, Patrick Assenga, Mshewa Karua, Khadija Mwago, Pendo Mwasomola, Cesilia Michael, Happy Abdallah, Stephen Kitomali na Paulo Makali.

Mdee, Bulaya, Msigwa na Heche Kisutu

Pia, wamo, Athumani Hassan, Omary Milodo, Emmanuel Ignastemu, Stephen Kitomali, Hamis Yusuph, Juma Juma, Mustafa Lada, Emmanuel Zakaria na Steven Ezekiel.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na maahtaka saba likiwemo la kukaidi amri halali kutoa lugha ya maudhi na kiharibu gari Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa shtaka la kwanza, tarehe 13 Machi 2020 washtakiwa wote kwa pamoja wakiwa katika gereza la Segerea lililopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, walikaidi amri halali na kwa makusudi walikaidi amri iliyotolewa na askari B 3648 SGT John ambaye aliwataka wahusika hao kuondoka eneo hilo la magereza na alikuwa akitimiza wajibu wake aliyopewa.

Katika shtaka la pili la kufanya mkusanyiko usio halali, Inadaiwa tarehe hiyo katika eneo la gereza la Segerea, washitakiwa wote kwa pamoja, walikusanyika katika eneo hilo la magereza isivyo halali hali iliyosababisha kuleta hofu na kuhatarisha amani na utulivu kwenye eneo hilo.

Shtaka la tatu la kuharibu mali, inadaiwa siku hiyo, washitakiwa wote kwa pamoja walishirikiana kufanya uharibifu wa geti la Segerea ambalo ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shitaka la nne la kutoa lugha ya kuudhi ambalo linamkabili Mdee, Inadaiwa siku hiyo katika gereza la Segerea, alitoa maneno ya kuudhi kwa askari magereza Sajenti B 3648 John, maneno ambayo yalipelekea uvunjifu wa amani.

Aidha katika shitaka la tano nalo lakutoa lugha ya kuudhi ambalo linamkabili Bulaya, inadaiwa tarehe hiyo ya tarehe 13 Machi 2020 mshitakiwa huyo akiwa maeneo ya gereza la Segerea alitoa maneno ya kuudhi kwa Sajenti B 3648 John na kupelekwa uvunjifu wa amani.

Shtaka la sita linalomkabili Jacob, inadaiwa mshitakiwa huyo siku hiyo akiwa eneo la gereza la Segerea alitamka maneno ya kuudhi kwa Sajenti B 3648 John.

Katika shitaka la mwisho, inadaiwa siku hiyo mshitakiwa Jacob alifanya shambulio kwa askari magereza kwa kumkunja na kumvuta shati askari huyo wakati akitekeleza majukumu .

Hakimu Shaidi amewataka washtakiwa hao wawahi kufika siku ya usikilizwaji wa shauri lao.

“Mnatakiwa muwahi kesi itasomwa saa 2.30 asubuhi, atakayechelewa mtu kufika mahakamani atawajibika,” amesema Hakimu Shaidi wakati akiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 28, Agosti 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!