Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wakiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam

Kesi ya Mbowe, Matiko yalala tena, Mawakili wavutana

JAJI wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, amepanga kutoa umauzi wa pingamizi la awali kwenye kesi iliyofunguliwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Uamuzi wa Jaji Rumanyikwa umetokana na hatua ya upande wa mashitaka kuweka pingamizi kuhusiana na rufaa.

Upande wa utetezi kesi ya rufaa ya pingamizi la kufutiwa dhamana umedai hakuna mahali walipoeleza kifungu cha sheria wakati wakitoa notisi ya kukata rufaa.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala, akijibu hoja za upande wa Jamhuri, amedai kuwa walitakiwa kuwasilisha rufaa chini ya kifungu cha sheria namba 359 na 361 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai.

Kibatala amedai kwamba suala la mwenendo wa kesi kuwa haujachapwa lilishatolewa uamuzi jana na Jaji Rumanyika na wakakubali ziletwe kama zilivyo.

Alidai mahakama ilitoa haki ya kusikiliza pande zote mbili katika suala la mwenendo wa kesi.

IMG-20181129-WA0034

Kibatala alisema rufaa yao ina msingi hivyo aliomba isikilizwe ili washtakiwa wapate haki yao ya kikatiba ya kuwa nje kwa dhamana.

Jaji Rumanyika baada ya kusikiliza hoja zote mbili aliahirisha kesi hadi kesho kwa ajili ya kutoa uamuzi wa pingamizi la Jamhuri la kutaka rufaa itupwe.

JAJI wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, amepanga kutoa umauzi wa pingamizi la awali kwenye kesi iliyofunguliwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko. Anaripoti Faki Sosi ... (endelea). Uamuzi wa Jaji Rumanyikwa umetokana na hatua ya upande wa mashitaka kuweka pingamizi kuhusiana na rufaa. Upande wa utetezi kesi ya rufaa ya pingamizi la kufutiwa dhamana umedai hakuna mahali walipoeleza kifungu cha sheria wakati wakitoa notisi ya kukata rufaa. Wakili wa utetezi Peter Kibatala, akijibu hoja za upande wa Jamhuri, amedai kuwa walitakiwa kuwasilisha rufaa chini ya kifungu cha sheria namba 359 na 361 cha…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram