Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Mahakama yakubali ushahidi wa Jamhuri 
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Mahakama yakubali ushahidi wa Jamhuri 

Viongozi wa Chadema wakijadiliana na wakili wao mahakamani Kisutu katika muendelezo wa kesi yao
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Julai 2019, imepokea kielelezo cha kamera ya kurekodi video na tepu vilivyowasilishwa na Jamhuri. Anaripoti Faki Sosi (endelea).

Kielelezo hicho kilichopingwa mahakamani hapo na upande wa utetezi, katika kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chadema. 

Viongozi wa chama hicho wanatuhumiwa kufanya uchochezi. Viongozi hao ni Freeman Mbowe, mwenyekiti Taifa; Dk.Vicent Mashinji, Katibu Mkuu: John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu-Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu-Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mwenyekiti wa Bawacha-Taifa; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya hiyo ametoa uamuzi huo baada ya kupitia hoja pande za zote mbeli.

Hakimu Simba amesema, ni kwa namna uhifadhi wa kidhibiti hiko na kwamba Kifungu cha 18 cha sheria ya elektoniki hakijaweka sharti la kiapo na kwamba ushahidi wake, umekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwenye kifungu hiko.

Kamera hiyo imepokewa kama kielelezo namba nne ambapo tepu mbili zimenukuliwa kama kielelezo namba 5.

Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018, upande wa Jamhuri unawakiliswa na Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu; Paul Kadushi, Wakili wa Serikali Mkuu; Dk. Zainab Mango, Wakili wa Serikali Mkuu; Wankyo Simon, Wakili wa Serikali Mwandamizi na Salim Msemo.

Upande wa utetezi umeongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.

Awali, wakili Kibatala alipinga kupokewa kielelezo kwa kudai, ushahidi wa kieletroniki hauwezi kupokelewa mahakamani mpaka kuwepo kwa kiapo mahususi juu ya utoaji wa vielelezo hivyo, kwa mujibu wa sheria fungu la 18 na 19 ya ushahidi wa kieleketroniki.

Dk Zainab alijibu hoja hizo kwa kuieleza mahakama, aina ya utunzaji vielelezo vilivyowasilishwa na shahidi wao ulikuwa mzuri kama yalivyo matakwa ya kisheria.

“Ni raia ya upande wa Jamhuri tumefanikiwa kukidhi matakwa yote ya sheria kifungu cha 18 (2) cha sheria ya ushahidi wa kieletroniki, yanayotaka vielelezo vitunze vizuri kabla kuwasilishwa mahakamani ambapo shahidi wa Jamhuri, aliielezea mahakama namna aliyovitunza vielelezo hivyo,” alieleza Dk. Zainabu.

Alidai, matakwa ya sheria juu ya ushahidi huo ni pamoja na kutunzwa na kuhifadhiwa kwa vidhibiti vya kieletroniki na mtu akiyehusika kwenye kuchakata vielelezo hivyo, na vifaa vilivyotumika viwe vizima bila kutumika mahala kwingine.

Dk. Zainabu aliendelea kudai, Kifungu cha 18 kinahitaji kitu kitachouthibitishia mahakama juu vielelezo hivyo na kwamba, ushahidi unaweza kutolewa kwa maneno, nyaraka au hati ya kiapo.

Akirejee kesi iliyotajwa na Kibatala, ya Exim Bank na Kilimanjaro Cofee Company Limited kesi namba 29 ambayo iliamuriwa mwaka 2013, kabla ya marekebishonya sheria ya ushahidi wa kieletroniki.

Kesi hiyo inahusu masuala ya kibenki na kwamba ipo sheria mahususi yanayohusu masuala ya benki ambayo ni kifungu cha 78 (A) sambamba na fungu la 79.

Pia akarejea kesi ya Emmanuele Mwasonga, ambayo ushahidi wa simu ulikataliwa mahakamani kutokana, namna ulivyohifadhiwa ambapo simu ile iliyorekodi sauti ilimrushia mtu mwengine na baadaye ile simu iliyorekodi kupotea.

Sauti ikiweka kwenye CD, na baadaye kupelekwa mahakamani, kutokana na mlolongo huo, ilikataliwa kwa ushahidi kutokana utunzaji wa kifaa kilichirekodi ushahidi.

Akiendelea kujibu pinganizi hilo Wakali Kadushi aliieleza mahakama, ushahidi uliotolewa umekidhi vigezo na matakwa ya kifungu cha 18 (2), (a), (b)na (c).

Alidai, matakwa ya sheria yana kigezo cha kifaa kilichohifadhi ushahidi kuwa kinafanya kazi wakati wote.

Kadushi alidai mahakamani hapo, hoja yao ya pili kuwa, suala la hati ya kiapo, ushahidi wa kurekodiwa kwenye mashauri ya jinai, hakuna hitajio la kisheria linalotaka utolewaji wa ushahidi wa kieletroni utolewa kwa hati ya kiapo. Na sio kifungu cha 18 wala kifungu kingine chochote.

Kadushi alisitiza, katika mashauri ya madai, ni jambo la kawaida ushahidi kuwasilishwa kiapo ambapo kwa mashauri ya jinai, mahakama inapokea kwa njia ya maneno.

“Sisi tunawasilisha kuwa kuwepo kwa hati ya kiapo sio hoja, tunaiomba mahakama yako isizingatie kabisa mapingamizi yaliyowasilishwa na wenzetu na ipokee vielelezo vilivyotolewa na shahidi,” aliwasilisha Kadushi.

Kibatala akijibu hoja hizo aliendelea kusisitiza, katika kutoa ushahidi wa kieletroniki, licha ya shahidi kutoa ushahidi wake mkuu, lazima kuwepo kwa kiapo mahususi kwa ajili ya kutoa ushahidi wa kieletroniki.

“Sheria ya kieletroniki imelenga hasaa mahakama kuu kitengo cha biashara na hata utungwaji wa sheria hiyo, umetokana na mashauri ya kibiashara kwenye mahakama.

“Hivyo, tunabomoa hoja Dk. Mango kuwa eti kwasababu uamuzi wa kesi ya Exim Benki umefanywa kabla ya marekebisho ya sheria ya eletroniki, sheria haielei hewani” amedai.

Kibatala alidai, ushahidi huo ungeweza kukubaliwa kwa mujibu wa sheria labda kutoka kwenye CCTV kamera au kwa mwandishi wa habari lakini shahidi huyu anatoka kwao (Jamhuri).

Alisisitiza, tafsiri ya ‘au’ ‘na’ (‘And’ & ‘Or’) kwenye kifungu cha 18 kimetumiwa vibaya na wakili Kadushi na kwamba hitaji la fungu la 18 (a) na (b), visomwe kwa pamoja kwamba vielelezo vile vingetolewa endapo vinamilikiwa na washtakiwa.

Mwasipu akiunga mkono hoja za utetezi alieleza, shahidi wa sita ni ofisa wa polisi aliyekuwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa Upulelezi Mkoa wa Kinondoni, ambaye ana maslahi kwenye shauri hili.

“Tulitegemea waje waandishi wa habari watoe ushahidi huu,” amesema.

Akirejea kwenye kesi ya uchaguzi ya Mwasonga, ambayo shahidi wa sita aliwalisisha mahakamani hapo kielelezo cha sauti ambacho mahakama kilikikataa kutokana shahidi huyo kuwa na maslahi na kesi hiyo.

Alikuwa ni mfuasi wa Chadema na alikuwa akitolea ushahidi kesi inayomuhusu mwanachama mwenzake (Mwasonga), katika Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!