Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Lissu & Ndugai sasa yaanza kuiva
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Lissu & Ndugai sasa yaanza kuiva

Mawakili wa Tundu Lissu wakitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania
Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga kuanza kusikiliza shauri la madai lililofunguliwa na Alute Mughwai, kupinga kuvuliwa ubunge kwa Tundu Lissu, aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Alhamisi ijayo. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Akisoma uamuzi wake mahakamani hapo, leo tarehe 15 Agosti 2019, Jaji Sirilius Matupa amesema, amechukua maamuzi hayo kwa kuzingatia hoja za kisheria na zile za kikatiba.

Amesema, “shauri hili limeletwa mahakamani kwa hati ya dharura. Hivyo basi, kwa kuzingatia kanuni zetu, mahakama inapaswa kusikiliza ombi hilo ndani ya siku 14 na kulimaliza.”

Aidha, Jaji Matupa amesema, “kwa kuzingatia kuwa maombi haya yanagusa haki ya ubunge wa mwombaji na kwa kuzingatia Bunge linatarajiwa kuanza hivi karibuni, nitasikiliza shauri hilo siku hiyo ili kuhakikisha kesi iliyopo mbele yangu inamalizika ndani ya muda huo.”

Alute kwa niaba ya ndugu yake, Tundu Antipas Lissu, amefungua shauri hilo mahakamani, kupinga hatua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kumvua ubunge wake Lissu.  Washitakiwa kwenye kesi hiyo, ni Spika Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Spika Ndugai aliliambia Bunge, 28 Juni mwaka huu, kuwa Lissu amepoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge. Alisema, amelazimika kuchukua uamuzi huo, kutokana na mwanasiasa huyo kutohudhuria mikutano ya Bunge kwa muda mrefu bila kutoa sababu.

Lakini Lissu kupitia kwa kaka yake Alute anasema, amevuliwa ubunge bila kuelezwa sababu na kinyume na sheria na Katiba ya Jamhuri.

Akieleze mamia ya watu waliofika mahakamani kusikiliza shauri hilo, Jaji Matupa alisema,“hii ni kesi inayofuatiliwa na mamilioni ya wananchi. Ni lazima mahakama itimize wajibu wake wa kuimaliza mapema.”

Ameagiza upande wa wajibu maombi kuwasilisha hati ya kiapo pinzani, tarehe 21 Agosti na waombaji (Alute Mughwai), kujibu siku inayofuata – tarehe 22 Agosti 2019.

Jaji Matupa alitoa maamuzi hayo, kufuatia kuibuka kwa mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa Spika Ndugai na wale wa serikali kwa upande mmoja na wale wa Alute.

Katika shauri hilo, wadaiwa hao wawili – mwanasheria mkuu wa serikali na Spika wa Bunge – wanawakilishwa mahakamani na mawakili Vicent Tangoh, Lucas Malunde na Mark Mulwambo. 

Naye Alute, aliwakilishwa mahakamani na mawakili wa kujitegemea, Pater Kibatala, Jeremiah Mtobesya, Omari Msemo, na Fred Kalonga.

Mawakili hao wa serikali, waliomba mahakama kuwapatia siku  nane kujibu madai ya mleta maombi, maelezo ambayo yalipingwa na Kibatara.

Katika maombi hayo, Lissu anaomba mahakama  kusimamishwa uapishwaji wa mbunge mteule wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu (CCM), hadi  shauri lake la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Mbali na kuomba zuio la kuapishwa kwa mbunge huyo, Lissu ameomba Mahakama Kuu kuliagiza Bunge kuwasilisha barua rasmi yenye uamuzi wa Spika wa Bunge kufuta ubunge wake.

Mawakili wanaomtetea Lissu kwenye shauri hilo, walitaka ombi kuhusu zulio dhidi ya Spika wa Bunge kutomuapisha mbunge huyo mteule, lisikilizwe leo, jambo ambalo lilipingwa na mawakili wa upande wa utetezi. 

Kufuatia mabishano hayo, Jaji Matupa ameamuru maombi yote kusikilizwa tarehe 23 Agosti (Alhamisi ijayo); upande wa  Jamhuri (wajibu maombi) walete majibu yao 21 Agosti na ikiwa upande wa wapeleka maombi wanataka kujibu majibu hayo, wanapaswa kufanya hivyo, tarehe 22 Agosti mwaka huu.

Amesema, baada ya usikilizwaji wa hoja hizo, 23 Agosti, ndipo mahakama itafanya maamuzi yake siku itakayopangwa, ambayo bila shaka itakuwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa 16 wa Bunge.

Akisisitiza msimamo wa mahakama hiyo Jaji Matupa amesema, amesikiliza hoja kutoka kwa pande zote mbili, na kwamba “consultations” na kuelezwa kuwa kabla ya 23 Agosti mwaka huu, hakuna kikao cha Bunge na hivyo mbunge huyo mteule hatakuwa ameapishwa katika kipindi hiki.

Lissu alikuwa mbunge wa Singida Mashariki, baada ya kushinda nafasi hiyo kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.  

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!