Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Chadema: Nusura ‘kiwake’ Kisutu
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Chadema: Nusura ‘kiwake’ Kisutu

Spread the love

VURUGU, vuta nikuvute na kurushiana maneno vimetawala kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakati wa kusikiliza kesi ya viongozi wa Chadema. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya polisi kujaribi kuzuia baadhi ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingia katika chemba za mahakama hiyo kwa ajili ya kusubiri  hukumu ya viongozi wa chama hicho.

Polisi walilazimika kuwazuia wafuasi hao kwa maelezo, kwamba chumba cha mahakama hiyo kimejaa kutokana na watu kuwa wengi.

Kutokana na wafuasi wa Chadema kutokuwa tayari, lakini pia kujiridhisha kwamba nafasi ya kutosha ipo, waliendelea kuwa na msimamo wa kutaka kuingia ndani.

Kutokana na mvutano huo, polisi walilazimika kurudi nyuma na kuruhusu wafuasi hao kuingia.

Hata hivyo, Boniphace Jacob, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo (Chadema), pamoja na Gerva Lyenda, Ofisa Habari Chadema Kanda ya Pwani walitumika kutuliza wafuasi wao.

Leo tarehe 10 Machi 2020, mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya uchochezi Na. 112/2018 inayowakabili viongozi wa Chadema.

Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa, John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho, Halima Mdee, Mwenyrkiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba majira ya saa 4:30 asubuhi, lakini imesogezwa hadi saa 7:30 mchana.

Ulinzi umeimarishwa katika Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, huku mamia ya watu wakijitokeza kusikiliza hukumu ya viongozi wa Chadema.

Leo mhakama hiyo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya kesi ya uchochezi Na. 112/2018, inayowakabili vigogo hao wa Chadema.

Tofauti na siku za nyuma, polisi kadhaa wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wamezingira viwanja vya mahakama hiyo.

Maalim Seif Shariff Hamad, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ni miongoni mwa watu waliohudhuria kusikiliza hukumu ya kesi hiyo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE kwa taarifa zaidi kuhusu kesi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!