Kesi ya Bungo imeahirishwa – MwanaHALISI Online

Kesi ya Bungo imeahirishwa

KESI ya iliyofunguliwa na Kondo Bungo aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kupinga matokeo ya ubunge kwenye Jimbo la Mbagala iliyopangwa kusikilizwa leo kwenye Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, imeahirishwa. Anaandika Faki Sosi.
Wakili wa Issa Mangunu, Mbunge wa Jimbo la Mbagala ambaye ni Samson Mbamba, ameiomba mahakama kumuongezea muda wa kupeleka utetezi wa mteja wake kwa maandishi kama alivyotakiwa na mahakama hiyo.
Mahaka ilimtaka mshitakiwa  huyo awasilishe utetezi wake mahakamani tarehe 26 Januari mwaka huu ambapo hakufanya hivyo.
Akizungumza na MwanaHALISI Online, wakili wa mlalamikaji Juma Nassoro amesema kuwa, kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa leo imesogezwa mbele kutokana na kuwa leo ni siku ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Tanzania na kwamba, jaji anayeisikiliza kesi hiyo alikuwa kwenye maadhimisho hayo.
Kesi hiyo inayoendeshwa na Jaji Wilfredi Dynsobera iliyofunguliwa mwaka jana na Bungo ambapo msajili wa kesi mahakamani hapo amemkubalia ombi hilo wakili wa mlalamikaji ambapo atapeleka utetezi wa mshitakiwa tarehe 9 Februari mwaka huu.
KESI ya iliyofunguliwa na Kondo Bungo aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kupinga matokeo ya ubunge kwenye Jimbo la Mbagala iliyopangwa kusikilizwa leo kwenye Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, imeahirishwa. Anaandika Faki Sosi. Wakili wa Issa Mangunu, Mbunge wa Jimbo la Mbagala ambaye ni Samson Mbamba, ameiomba mahakama kumuongezea muda wa kupeleka utetezi wa mteja wake kwa maandishi kama alivyotakiwa na mahakama hiyo. Mahaka ilimtaka mshitakiwa  huyo awasilishe utetezi wake mahakamani tarehe 26 Januari mwaka huu ambapo hakufanya hivyo. Akizungumza na MwanaHALISI Online, wakili wa mlalamikaji Juma Nassoro amesema kuwa, kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa leo imesogezwa mbele…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube