Wataalam wa BVR wakiweka sawa mashine hiyo kabla ya kuanza kuandikisha wapiga kura

Kesho Arusha, Kilimanjaro kuanza rasmi BVR

UBORESHAJI wa Daftari la Wapiga Kura kwa njia ya Kielektroniki (BVR), katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha unatarajia kuanza rasmi tarehe 18 Julai 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo amesema Dk. Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) tarehe 15 Julai 2019 wakati alipohudhuria katika mafunzo ya waandikishaji wasaidizi wa zoezi hilo, jijini Arusha.

Dk. Kihamia amesema zoezi hilo katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha litafanyika kwa muda wa siku saba, na kutoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kujitokeza kujiandikisha kwa kuwa siku hizo zikimalizika, NEC haitaongeza muda wa ziada.

Dk. Kihamia amesema baada ya zoezi hilo kukamilika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, litahamia katika mikoa mingine, na kwamba NEC itaendelea kutoa taarifa na ratiba ya uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa njia ya Kielektroniki (BVR).

UBORESHAJI wa Daftari la Wapiga Kura kwa njia ya Kielektroniki (BVR), katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha unatarajia kuanza rasmi tarehe 18 Julai 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Hayo amesema Dk. Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) tarehe 15 Julai 2019 wakati alipohudhuria katika mafunzo ya waandikishaji wasaidizi wa zoezi hilo, jijini Arusha. Dk. Kihamia amesema zoezi hilo katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha litafanyika kwa muda wa siku saba, na kutoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kujitokeza kujiandikisha kwa kuwa siku hizo zikimalizika, NEC haitaongeza muda wa ziada. Dk. Kihamia amesema baada ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram