Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kaya 700 Monduli kunufaika na maji
Habari Mchanganyiko

Kaya 700 Monduli kunufaika na maji

Maji ya bwawa yaliyokuwa yanatumika na wakazi wa Monduli. Picha ndiogo mashine ya kuchuja maji
Spread the love

KAYA zipatazo 700 za Kitongoji cha Irmorijo katika Kijiji cha Emairete wilayani Monduli zilizokuwa zinatumia maji ya bwawa zinatarajia kunufaika na mradi wa kusafisha na kuchuja maji kuwa safi na salama uliozinduliwa kijijini hapo, anaandika Mwandishi Wetu.

Awali, wananchi hao walikuwa wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa maji hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo hilo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim, akizungumza juzi kwenye uzinduzi wa mradi huo alisema lengo ni jamii hiyo kunufaika na maji safi na salama yanayochujwa kupitia ubunifu wao.

Kim amesema pamoja na mradi huo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220.

Amesema Smart Vision kupitia uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency, (KOTRA) jamii ya eneo hilo itanufaika na mradi huo wenye lengo la kuondokana na matumizi ya maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa ya tumbo.

“Jamii ya eneo hili kupitia Mchungaji wa Kanisa la Enyorata, Daniel Vengei, walileta maombi kwetu kuwa wana tatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze kutatua hili suala la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na kusafisha maji,” amesema Kim.

Mkazi wa kitongoji hicho, Rose Lemomo, amesema awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama lakini kupitia mradi huo wataondokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakiwakabili hasa watoto.

Aliwashukuru wote waliohusika na kufanikisha mradi huo, kwani hivi sasa watakuwa wanachota maji bwawani na kuyachuja na kuyasafisha kupitia mitambo hiyo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Irmorijo, Mirishi Songoyo, alishukuru shirika hilo kwa kufanikisha mradi huo wa maendeleo ambao utainufaisha jamii ya eneo hilo walioteseka kwa muda mrefu juu ya suala la maji.

“Tunawaomba wananchi watakaofikiwa na mradi huu kuhakikisha wanawasaidia na wale ambao bado wanasubiri kupatiwa majiko na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji,” amesema.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Irmorijo, Stephen Laizer, aliwataka wananchi waliofanikiwa kupatiwa mradi huo kuhakikisha wanautunza ili kunufaika nao kwa muda mrefu kwani wameteseka kwa miaka mingi kwenye tatizo la maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!