Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kauli ya Mbowe, Zitto iliyomchefua Polepole, ataka wanyimwe kura
Habari za Siasa

Kauli ya Mbowe, Zitto iliyomchefua Polepole, ataka wanyimwe kura

Humphrey Polepole, Mbunge wa kuteuliwa na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

HATUA ya Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutaka wananchi wafungiwe ndani kuepuka maambukizi ya corona (COVID-19), limemkera Humphrey Polepole. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hata hivyo, Polepole ameeleza kushangazwa na hatua ya Mbowe kuagiza wabunge wa Chadema kutohudhuria bunge kwa madai kukaa kajiweka karantini kwa siku 14 ‘viongozi kama hawa wanimwe kura.’

Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, Zitto na Mbowe hawakuwa na dhamira njema, na kwamba walifanya vile kwa kuwa wanalipwa mishahara kila mwisho wa mwezi.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 22 Mei 2020, katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, jijini Dar es Salaam Polepole amesema, uamuzi uliofanywa na Rais John Magufuli kutofungia ndani wananchi (lockdown), dunia imejifunza kutoka kwake.

“Wapo watu hapa Tanzania, ni vizuri mkawafahamu kutoka vyama vya upinzani, baadhi yao walitaka tufungiwe ndani. Halafu tukifungiwa ndani, nauliza mama lishe wangepata chakula wapi?

“…hivi Zitto anaposema sisi tufungiwe, si ana mshahara yule wa milioni kadhaa! Hata akijifungia ndani, atanunua vitu kwa M-Pesa na TigoPesa na wenzake wote. Vipi mamalishe wa Kibirizi? vipi mamalishe wa Kigoma Ujiji? Akafungiwe ndani, na yeye anapokea mshahara?” amehoji Poplepole.

Amesema, licha ya kutaka watu wafungiwe ndani, hakusema namna gani watu ambao hawana mshahara wanaweza kupata kipato chao na kwamba, Serikali haiwezi kulipa mishahara kwa watu milioni 55 waliopo nchini.

“Akatoka ndugu Mbowe, tunamfahamu na mimi namshukuru sana kwasababu hata wabunge awake wamelidhihirisha hilo. Yule bwana, kiongozi wa kiimla…, yule ni kiongozi wa kiimla kweli kweli.”

“…sasa Mbowe anamwambia kila mbunge wake ‘kuanzia leo sasa mtakaa nyumbani, mimi sikumshangaa Mbowe kwasababu hata rais alipokuwa anazindua Bunge awamu hii ya tano (tarehe 20, Novemba 2015), aliwaambia ‘simama toka nje.’ Wale jamaa wakasimama wakatoka nje, na wakati mwingine akawaambia funga mdomo kwa plasta, wakafunga mdomo na plasta.”

Hata hivyo, amesema, licha katikati ya beza zao, Rais Magufuli aliendelea kulitia moyo ataifa kwa kuendelea kufanya kazi bila kupuuza maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Wizara ya Afya.

“Nchi kadhaa, ilikuwa ukionekana barabarani, basi utatembezewa bakora, manyanyaso na mambo kama hayo, Rais Magufuli aliliona hili mapemba na akatambua akili za kuambiwa, changanya na za kwako,” amesema na kuongeza “mbinu zao (mataifa ya nje) kwa hakika haziwezi zikatumika hapa kwetu.”

Polepole amesema, CCM na Serikali yake wanayo kila sababu ya kutangaza ushindi dhdi ya hofu ya virusi vya corona,“tunamshukuru Rais Magufuli kwa kututoa hofu na kuendelea kutuvusha na majanga mbalimbali kama hili. Chama Cha Mapinduzi tunasema asante baba.”

Pia, Polepole ametoa pongezi kwa viongozi wa dini wa madhehebu yote, wauguzi, madaktari na watumisho wote wa afya kwa kujitoa kusaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!