Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kauli ya JPM, LHRC yatoa tahadhari
Habari za Siasa

Kauli ya JPM, LHRC yatoa tahadhari

Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), kimetoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha dhana ya makubaliano ya kukiri kosa, inatumika kwa usahihi katika mchakato wa upatikanaji haki. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 25 Septemba 2019 na LHRC kupitia kwa Wakili Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho.

Taarifa ya LHRC inaeleza kuwa, mabadiliko hayo ya Sheria ya Makosa ya Jinai kupitia Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria yaliyotoletwa kupitia Muswada namba 4 wa mwaka 2019, yanatakiwa kutekelezwa kwa kuzingatia Katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa.

“Kutoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha dhana ya Makubaliano ya Kukiri Kosa (Plea Bargaining) inatumika kwa usahihi katika mchakato wa upatikanaji haki nchini, kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na Mikataba ya Kimataifa ya Haki za Binadamu,” inaeleza taarifa ya Wakili Henga.

Pia, LHRC imeshauri makubaliano hayo yafanyike bila shuruti wala masharti yoyote yaliyo nje ya sheria, hali kadhalika mshtakiwa anatakiwa kuwa huru kadri atakavyoona inafaa kabla na wakati wa kufanya makubaliano hayo.

Vile vile, LHRC imeshauri nafuu hiyo ya kisheria itumike kwa washtakiwa wa makosa mbalimbali bila kujali kiwango cha pesa au aina ya kosa bila kuathiri sheria. Pia, utaratibu huo uzingatie sheria.

Kuhusu ufafanuzi wa kisheria wa makubaliano hayo, Wakili Henga amesema makubaliano hayo ni maalumu katika kesi ya jinai kati ya mwendesha mashtaka na mshtakiwa, na kuwa mshtakiwa anakubali kukiri kosa moja au zaidi katika makosa aliyoshtakiwa nayo ili apate nafuu ya kesi husika.

“Pia, mshitakiwa anaweza kukubali kutoa ushirikiano kwa Mwendesha Mashtaka utakaowezesha  kupatikana kwa taarifa zinazohusiana na kosa hilo aliloshitakiwa nalo,” inaeleza taarifa ya LHRC na kuongeza;

“Mwendesha Mashtaka baada ya kufanya mahojiano na mtu aliyetendewa kosa au Mpelelezi wa kesi hiyo, anaweza kuingia katika makubaliano maalumu na mshtakiwa na Wakili wake kuhusu kosa hilo.”

Hata hivyo, taarifa hiyo imefafanua kwamba nia ya kuanza kufanya makubaliano hayo itatakiwa kupelekwa Mahakamani kwa ajili ya taarifa, ingawa Mahakama haitohusika katika majadiliano hayo.

LHRC imeeleza taratibu zinazofanyika katika makubaliano ya kukiri kosa, ikiwemo makubaliano ya maandishi yanayojumuisha taarifa zote  muhimu zitakazojadiliwa katika kesi husika, makubaliano hayo husomwa kwa lugha ambayo mshtakiwa anaielewa.

Pia, makubaliano hayo yanatakiwa kukubaliwa na mshtakiwa pamoja na kutiwa saini na mwendesha mashtaka, mshtakiwa na wakili wa amshtakiwa kama anaye.

Vile vile, kituo hicho kimefafanua kwamba mshtakiwa hatokuwa na haki ya kusikilizwa na mahakama na kutoa utetezi au ushahidi juu ya kosa husika. Hatokuwa na haki ya kukata rufaa kuhusu uendeshaji wa kesi yake isipokuwa anaweza kukata rufaa kupinga utaratibu uliotumika wakati wa kutolewa hukumu.

LHRC imeeleza wajibu wa mahakama katika makubaliano, na kuwa mahakama itatakiwa kujiridhisha kwamba makubaliano hayo yamefanyika bila shuruti, kuyasajili makubaliano, kutamka maamuzi ya makubaliano hayo au kutoa maamuzi endapo kuna ulazima wa kuyatoa au kukataa makubaliano hayo kwa sababu za msingi.

Mahakama itaweka katika kumbukumbu za mahakama makubaliano hayo endapo yatakubaliwa na mahakama kwa kufuata taratibu maalumu.

LHRC imeainisha makosa yasiyoruhusiwa kufanyiwa makubaliano maalumu ya kukiri kosa, ikiwa pamoja na makosa ya udhalilishaji wa kingono yenye adhabu ya kufungwa zaidi ya miaka mitano au udhalilishaji dhidi ya mtu aliyechini ya umri wa miaka 18.

Makosa mengine ni uhaini, kumiliki au kusafirisha madawa ya kulevya yenye thamani inayozidi shilingi milioni 10, ugaidi, kumiliki nyara za serikali zenye thamani inayozidi shilingi milioni 10 biila idhini ya mkurugenzi wa mashtaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!