Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wizara ya Mambo ya Nje kutifuana
Habari za SiasaTangulizi

Wizara ya Mambo ya Nje kutifuana

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Faraji Mnyepe amemtoa wasiwasi Rais John Magufuli kuhusu kibarua alichompa cha kuirekebisha wizara hiyo, huku akiahidi kuutumia waraka wa rais wa mwaka 1964 katika kutatua changamoto zake. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akizungumza baada ya kuapishwa leo tarehe 3 Oktoba 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam, Dk. Mnyepe ameeleza kuwa, waraka huo unaelekeza  mwongozo bora wa kuendesha Wizara ya Mambo ya Nje ikiwemo kueleza jinsi wizara hiyo itakavyoshirikiana na wizara nyingine za hapa nchini, mabalozi na jumuiya za kimataifa.

“Ukisoma waraka wa rais wa mwaka 1964 unatoa maelekezo ya namna ya wizara ya mambo ya nje itakavyofanya kazi na wizara nyingine na mabalozi na jumuiya za kimataifa, waraka ule ni moja ya vitu nitakavyoenda kusimamia ninaamini unajenga utaratibu wa kazi kati ya wizara na wizara nyinge, na mabalozi walioko nchi za nje,” amesema Dk. Mnyepe.

Dk. Mnyepe ameahidi kufanya kazi kwa mujibu wa kiapo chake pamoja na kufuata sheria, taratibu na kanuni za sheria za nchi.

“Ujasiri huu nitauzingatia, kwa wale watanzania ambao wana wasiwasi, kwa maana ujumbe nilioupata kutoka kwako kwamba kazi ni ngumu. Nikutoe hofu naenda kufanya kazi, naenda kufanya kazi kama kiapo kilivyosema kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za sheria ya Jamhuri ya Muungano, sina wasiwasi na idhini yako uliyonipa niende kufanya kazi maana nilisikia ulipomuapisha naibu waziri, ulisema wazi kwamba wizara ile haikufurahishi, ulitoa sababu na sababu zile ni za kweli zote,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!