Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Katazo mifuko ya plastiki: Wananchi watakiwa kubeba vyombo vyao
Habari Mchanganyiko

Katazo mifuko ya plastiki: Wananchi watakiwa kubeba vyombo vyao

Spread the love

WANANCHI wameshauriwa kwenda dukani au sokoni na vyombo vya kubebea bidhaa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya katazo la mifuko ya plastiki kuanza ikiwa ni pamoja na adhabu ya faini ya shilingi 30,000. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 10 Mei 2019 na Ally Mfinanga, Ofisa Mazingira wa Jiji la Dodoma ambaye ni mjumbe wa kikosi kazi cha Taifa cha utekelezaji agizo la serikali la katazo la mifuko ya plastiki.

Mfinanga amesema, kutokana na katazo la serikali la kutumia mifuko ya plastiki ifikapo Juni 1 mwaka huu, amewashauri wananchi kubeba vyombo yenye uwezo wa kuhimili maji na unyevunyevu kama kubebea samaki wa bichi na nyama.

“Kwa sasa, baadhi ya watengenezaji mifuko mbadala tayari wameishatengeneza, lakini ukiiangalia ile mifuko, inaonekana kutokuwa na uwezo wa kubeba kitu kibichi kwasababu unalowana na kuchanika,” amesema Mfinanga.

Akizungumzia jinsi ya kuwafikishia taarifa wananchi Mfinanga amesema, wanawatumia watendaji wa kata, viongozi wa dini, taasisi, shule na masoko kwa kuwapelekea barua za katazo la mifuko ya plastiki.

“Tunatumia sehemu ambazo zinamikusanyiko mingi kwasababu taarifa inafika kwa watu wengi kwa haraka, mfano kwenye kanisa ni rahisi kiongozi wa dini kuwafikishia taarifa waumini wake na watu wengi wakapata taarifa,” amesema Mfinanga.

Amesema, serikali itaeleza ni wapi itapelekwa rasmi mifuko yote iliyopo madukani itakayokusanywa ifikapo tarehe ya mwisho ya matumizi ya mifuko hiyo.

“Kwasasa mifuko yote itakayokusanywa ifikapo Mei 31 mwaka huu, itahifadhiwa katika ofisi za kata hadi hapo litakapopatikana eneo linguine,” amesema.

Hata hivyo amesema, sheria ya usimamizi wa mazingira wa mazingira zitatumika, sheria ya hifadhi ya usimamizi wa mazingira namba 20 ya mwaka 2004 imeainisha viwango vya faini.

“Mtumiaji atakayekiuka sheria faini shilingi 30,000, atakayeingiza nchini faini shilingi milioni 20, atakayesafirisha kupeleka nje ya nchi faini shilini milioni 20 na atakayekutwa anazalisha au kusambaza faini shilingi milioni 10,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!