Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kanisa lanufaisha vijana 6,000 Arusha
Habari Mchanganyiko

Kanisa lanufaisha vijana 6,000 Arusha

Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu
Spread the love

KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewanufaisha kwa elimu ya malezi ya maadili mema zaidi ya vijana 6,000 itakayowawezesha kuwa na utu na kulea vema familia, anaandika Mwandishi Wetu.

Askofu Mkuu wa jimbo hilo, Josephat Lebulu, amesema hayo alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za upadrisho wa mapadri watatu zilizofanyika Kanisa Katoliki Burka jijini hapa.

Amesema jimbo hilo linapenda kuwaanda viongozi wakiwa wadogo kupitia shule za seminari za jimbo hilo ikiwemo ya Usa River ambayo ni kwa ajili ya wavulana pamoja na ya seminari iliyopo Kisongo ambayo ni ya kuwaandaa wasichana wa kike ili waweze kukua katika maadili mema.

Amefafanua mmomonyoko wa maadili yanazidi kumomonyoka katika jamii kutokana na wazazi kushindwa kusimamia malezi ya watoto na kwamba wao kama kanisa wamejiwekea utaratibu wa kuelimisha vijana ambao wamemaliza darasa la saba ili kuwajengea maadili ambayo yatawajenga katika utu na hatimaye kuwezesha familia kujua

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miito wa jimbo hilo, Fulgence Mallya, amesema kupatikana kwa mapadri hao ni neema kwani awali ilikuwa changamoto na wataweza kusaidia kanisa hilo kuwahudumia watu wengi.

Amesema jimbo hilo limekaa miaka mitano bila kupata watumishi na kwamba kufanikiwa kupata mapadri watatu kutasaidia parokia zinaongezeka kupata wahudumu na pia kuweza kuwafikia watu wanaohitaji huduma katika jamii tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Jimbo letu limekaa muda wa miaka mitano bila kupata mapadre wapya hivyo naamini mapdri hawa watahudumia parokia zetu lakini hata kuhudumia watu kwani watu nao wanazidi kuongzeka lakini watenda kazi ni wachache zaidi,” amesema.

Aidha, amesema wakristo wanapaswa kuendelea kusali kumwomba Mungu ili zile mbegu ya wito zinazosiwa na mungu katika familia ziendelee kukua na hatimae waendelee kupata mapadri wa ukweli ambao watawezesha kubadilisha ulimwemgu ambao unaegemea maadili maovu yaliyopotoka ili kwa pamoja kanisa liweze kuleta mabadiliko katika jamii.

Amewataja mapadre waliopadrishwa kuwa ni pamoja na Alfred Fadhili, Kariuki Ndege pamoja na Padre Emanueli Swai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!