Lugola ametoa kauli hiyo, alipoulizwa msimamo wa wizara yake juu ya kupotea mwandishi huyo, Novemba mwaka jana.
Lugola amesema wizara yake haiingilii uhuru wa mtu kwani kitendo cha mtu kuondoka nyumbani kwake na kuelekea pasipojulikana kwani sheria za nchi hazimzuii mtu kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwani kufanya hivyo si kuvunja sheria.
Waziri Lugola amesema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.
“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” amesema.
Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). “Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka,” alisema Lugola
Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.
Jeshi la Polisi, ambalo jukumu lake kubwa ni kulinda watu na mali zao, liko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Leave a comment