Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Kampeni uchaguzi Yanga kuanza leo
Michezo

Kampeni uchaguzi Yanga kuanza leo

Jengo la Yanga
Spread the love

KUELEKEA uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga 13 Januari, 2019 Kamati ya Uchaguzi ambayo ipo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza leo 8 Januari, kufunguliwa rasmi kwa kampeni kwa wagombea wa nafasi nafasi za Mwenyekiti, Makamo M/nyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, uliopo Masaki jijini Dar es Salaam unaonekana kuwa wa sintofahamu kwa wanachama wa klabu hiyo kutokana na mwitikio wao kuwa mdogo katika kushiriki suala hili.

Hali hiyo inataokea baada ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kutotaka uchaguzi wao kusimamiwa na TFF kutokana na kuamini kuwa Yanga ina katiba yake pamoja na kamati ya uchaguzi hivyo inapaswa kuendesha mambo yao wenyewe licha ya kushindwa kufanya uchaguzi kwa wakati.

Mjumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga, Suzan Lyimo ambaye alimwakilisha makamu Mwenyekiti kwenye mkutano huo amesema kuwa ni wengi wanapotoshana kwamba kunauwezekano wa kuwepo kwa vurugu au uvunjifu wa amani katika uchaguzi huo lakini uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

“Leo ni tarehe 8 Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi amekusudia kutangaza ni siku ya uzinduzi wa kampeni, tarehe 13 ni siku ya uchaguzi ni wengi wanapotoshana kutakuwa na vurugu au kutajitokeza vitu ambavyo vya kutishia amani, Hapana, uchaguzi utakuwa huru na haki,” alisema mjumbe huyo.

Aidha Lyimo alipenda kuwaasa wanachama wa Yanga ambao hawajahakiki wala kulipia kadi zao waende kwenye matawi yao ili kukamilisha suala hilo ili kuepusha usumbufu siku hiyo.

Wagombea ambao wanaingia kwenye kinyang’anyiro hicho katika nafasi ya Mwenyekiti ni Dkt. Jonas Tiboroha, Mbaraka Igangula na Erick Ninga. Kwa wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu, waliopitishwa ni pamoja na, Yono Kevela, Titus Osoro na Salum Chota.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, waliopitishwa ni 16 ambao ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.

Ikumbukwe Yanga wanaingia kwenye uchaguzi huo ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi baada ya kujiuzuru kwa aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji, Clement Sanga ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti, Salum Mkemi, Hashimu Abdallah, Ayub Nyenzi na Omary Said.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!