Kamishna wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere

Kamishna wa TRA anusurika ajalini Dodoma

KAMISHNA wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere amepata ajali asubuhi ya leo tarehe 11 Septemba 2018 mkoani Dodoma baada ya gari lake kugongana na gari jingine. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, RPC Girres Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa, hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo au majeruhi.

Ajali hiyo imetokea eneo la Nanenane jijini Dodoma ambapo gari la serikali aina ya V8 alilokuwamo Kichere, kugongana na gari binafsi.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa, gari la serikali lilikuwa linajaribu kulipita gari jingine kwenye njia panda ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) ambapo gari binafsi likajitokeza kwa mbele wakati likielekea UDOM.

KAMISHNA wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere amepata ajali asubuhi ya leo tarehe 11 Septemba 2018 mkoani Dodoma baada ya gari lake kugongana na gari jingine. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea). Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, RPC Girres Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa, hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo au majeruhi. Ajali hiyo imetokea eneo la Nanenane jijini Dodoma ambapo gari la serikali aina ya V8 alilokuwamo Kichere, kugongana na gari binafsi. Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa, gari la serikali lilikuwa linajaribu kulipita gari jingine kwenye njia panda ya kwenda Chuo Kikuu…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube