Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kagame, Museven wakaribia kuzichapa  
Kimataifa

Kagame, Museven wakaribia kuzichapa  

Spread the love

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame (62), amemtuhumu “swahiba wake wa miaka mingi,” Rais wa Uganda, Yower Musseven, kwamba anapanga njama za kuangusha serikali yake. Anaripoti Yusuf Katimba … (endelea).

Akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa nchini mwake, Rais Kagame amesema, Rais Museven na serikali yake, wanaliunga mkono kundi la Rwanda National Congress (RNC), linalopinga serikali halali ya Rwanda.

Amesema, “kundi la RNC linapinga serikali halali ya Rwanda na linatumiwa na Uganda, kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea; na au kuishi nchini Uganda.

Taarifa zinasema, mgogoro wa sasa, waweza kusababisha mataifa hayo mawili yakaingia kwenye mapigano na kuna madai kuwa nchi zote mbili – Rwanda na Uganda – zimesogeza majeshi yake kwenye mipaka yao ili kujiandaa kwa lolote.

Amesema, vitendo vya Rais Museven kutaka kuangusha utawala wake, vimeanza miaka 20 iliyopita, na katika kuthibitisha hilo, amerejea yaliyomo kwenye kitabu kiitwacho, “From Genocied to Continental War.” Kitabu ambacho rais amefanya rejea, kiliandikwa na mwandishi wa vitabu ambaye ni rais kutoka Ufaransa, Gerard Prunier.

Kwa mujibu wa Rais Kagame, mwandishi huyo aliandika kwamba alikutana na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Seth Sendashonga mwaka 1998 akiwa na maafisa wakuu wa jeshi la Uganda na katika mazungumzo yao, walijadili jinsi ya kumsaidia Sendashonga ili kuangusha utawala wake.

Mwandishi huyo katika kitabu chake kulingana na maelezo ya Rais Kagame, serikali ya Uganda ilikuwa imemuahidi kumsaidia kijeshi.

”Sababu ya mimi kurejelea kuzungumza haya nimetaka kuwaonyesha mfululizo wa jinsi mambo yalivyokwenda mnamo miaka 20 iliyopita. Tulijaribu kufanya mikutano ya hapa na pale ili kutafuta suluhu, lakini hakuna suluhu iliyopatikana,” ameeleza Kagame.

Ameongeza, “ukweli ni kwamba Seth Sendashonga, alifariki dunia kwa kuwa alivuka mstari mwekundu. Sifurahii kusema hivyo, lakini pia sijutii kifo chake.”

Seth Sendashonga aliuawa katika mazingira ya kutatanisha mjini Nairobi mwaka 1998, alipokuwa uhamishoni baada ya kutofautiana na utawala wa Rwanda.

Rais Kagame amesema, mgogoro huo ulishika kasi hivi karibuni kufuatia wananchi wa Rwanda wanaoingia nchini Uganda au kufanyia kazi nchini humo, kushikwa na kuzuiliwa sehemu ambazo hazijulikani na kufanyiwa vitendo vya mateso.

Amesema, vitendo vyote hivyo vimefanywa kwa baraka za utawala wa Uganda na umetoa nafasi ya ushirikiano na kundi la RNC, ambalo linaongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, Jenerali Kayumba Nyamwasa.

”RNC wanafanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vya usalama vya Uganda. Kilicho wazi ni kwamba wanachokifanya ni kunyanyasa wanyarwanda ambao hawataki kuungana nao huku wakiwasingizia kwamba wametumwa na utawala wa Kigali kuhujumu usalama wa Uganda na kuuwa wanyarwanda wa upinzani.

“Madai haya hayana msingi hata kidogo. Lakini haya yote yanaonyesha ushirikiano wa dhati uliyopo baina ya serikali ya Uganda na kundi la RNC,” ameeleza Rais Kagame.

Rais Kagame amesisitiza kwamba mara kadhaa mwenyewe aliwasilisha malalamiko hayo kwa mwenzake Yoweri Museveni na kwamba hakuonyesha utashi wowote wa kuyatatua.

Wiki iliyopita serikali ya Rwanda ilikataza wananchi wake kwenda nchini Uganda na kusababisha mkwamo wa biashara.Rwanda inasema inatoa kipaumbele kwa maiasha ya raia wake zaidi kuliko biashara baina ya nchi mbili.

Hata hivyo, Uganda imekana madai hayo na kuongeza kuwa “ni Rwanda inayotuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi ya Uganda.”

Rais Kagame ambaye amewahi kuwa makamu wa rais na waziri wa ulinzi wan chi hiyo kati yam waka 1994 hadi 2000, amekuwa na migogoro ya mara kwa mara na majirani zake. Kati yam waka 2013 na 2015, alikuwa na mgogoro mkubwa na Tanzania na kabla ya kuibuka kwa mgogoro huu, taifa hilo lilikuwa na mgogoro mkubwa na Burundi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!