Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki

Kada wa CCM awavaa Zitto, Lissu, amsifia JPM

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC), Mussa Mwakitinya maarufu kwa jina la ‘Mwana wa Mungu’ amewashambulia wabunge wa upinzani na kueleza kuwa wana nia mbaya na amani ya taifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mwakitinya ambaye kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumzia na vyombo vya habari amesema kuwa wanasiasa hao ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe na mbunge wa Singida Mashariki Tindu Lissu.

Mnec huyo alisema kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakifanya siasa za kuliita doa taifa kwa kulitangaza vibaya na kuwadhalilisha viongozi wakuu wa nchi.

“Nataka ni mwambie Zitto kuwa anatakiwa kurudi jimboni kwake kwa maana watu wake wanapata shida sana na nataka nikuambie Zitto kuwa hauta kwa kuwa ana hali mbaya sana jimboni,mimi ni Mnec nazunguka nchi nzima najua hali aliyonayo ya kisiasa,” alisema Mwakitinya.

Katika mazunhumzo na waandishi wa habari Mwakitinya alimtaka Zitto kuendeleza siasa za ujumla na badala yake aridi jimboni kwake aka fanye sasa kwani bila kufudi jimboni hatarudi Bungeni tena.

Nataka nimwambie Zitto kuwa anatakiwa kurudi jimboni kwake kwa maana watu wake wanapata shida sana na nataka nkuambie Zitto kuwa hauta kwa kuwa ana hali mbaya sana jimboni, mimi ni Mnec nazunguka nchi nzima najua hali aliyonayo ya kisiasa,” alisema Mwakitinya.

Akizungumzia hali ya kisiasa ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu Chadema Mwakitinya alimtaka Lissu kurudi mapema jimboni na kama atachelewa atamkuta (Mwakitinya) akiwa mbunge wa Jimbo hilo.

Katika hatua nyingine Mnec huyo alisema kuwa anashangaa watu ambao wamekuwa na tabia ya kubeza Juhudi za Rais Dk John Magufuli.

Alisema hakuna kiongozi ambaye anaweza kufikia Rais wa awamu ya Tano kwa kufanya kazi nzuri na zenye maendeleo kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa anazo taarifa za siri kuwa yapo baadhi ya mashirika ambayo ya na wasaidia wanasiasa uchwara kufanya siasa chafu.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC), Mussa Mwakitinya maarufu kwa jina la 'Mwana wa Mungu' amewashambulia wabunge wa upinzani na kueleza kuwa wana nia mbaya na amani ya taifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma ... (endelea). Mwakitinya ambaye kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumzia na vyombo vya habari amesema kuwa wanasiasa hao ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe na mbunge wa Singida Mashariki Tindu Lissu. Mnec huyo alisema kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakifanya siasa za kuliita doa taifa kwa kulitangaza vibaya na kuwadhalilisha viongozi wakuu wa nchi.…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram