Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kada BAVICHA atoweka, Chadema wahaha kumsaka
Habari za Siasa

Kada BAVICHA atoweka, Chadema wahaha kumsaka

Bendera ya Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa wito kwa Jeshi la Polisi, vyombo vya dola na wananchi kumtafuta Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) wilayani Ilala, Michael Kapama aliyetoweka kwa siku tano sasa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, Katibu wa BAVICHA wilaya ya Ilala, Gevas Lyenda amesema viongozi wa Chadema kwa kushirikiana na familia ya Kapama, wametoa taarifa za kupotea kwake katika Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ambapo polisi wameanza kumtafuta.

“Familia imeshatoa taarifa za kupotea kwa Kapama katika Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, hawajatupa R.B wakisema kuwa suala lake halihitaji R.B na kuwaambia walete picha yake ili wasaidie kumtafuta,” amesema Lyenda.

Naye Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Patrick Ole-Sosopi amesema, viongozi wa baraza hilo wanawasiliana na familia ya Kapama katika jitihada za kumtafuta ndugu yao, ambapo ameomba vyombo vya dola na wananchi kutoa ushirikiano wao katika kumpata Kapama.

Kapama anadaiwa kupotelea kusikojulikana tangu usiku wa Jumapili ya tarehe 6 Januari 2019, ambapo mara ya mwisho alionekana katika eneo analofanyia biashara lililoko Feri jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!