Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jussa amsuta Kikwete hadharani
Habari za SiasaTangulizi

Jussa amsuta Kikwete hadharani

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete picha kubwa. Kulia ni Ismail Juma na kulia ni kikosi cha Zanzibar Heroes kilichotinga fainali michuano ya Chalenji
Spread the love

ALIYEKUWA Rais wa Jamhuri, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, “amesutwa” hadharani kuwa ndiye chanzo kikuu cha kuwapo mkwamo wa kisiasa, Visiwani Zanzibar. Anaandika Saed Kubenea… (endelea).

Tuhuma dhidi ya Kikwete zimetolewa leo Jumamosi (tarehe 16 Desemba) na Ismail Jussa Ladhu, mwanasiasa na kiongozi mashuhuri kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Akiandika katika mtandao wake wa twitter, Jussa anasema, Kikwete hawezi kuwa na dhamira njema ya kuitakia mema Zanzibar kwa kuwa ndiye kinara mkuu wa kuivuruga.

Kauli ya Jussa ilifuatia hatua ya rais huyo mstaafu kuipongeza timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Hories), inayoshiriki mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), nchini Uganda.

Akiandika katika ukurasa wake wa twitter, Kikwete alisema, “napongeza Zanzibar Heroes kwa kututoa kimasomaso na kutinga fainali. Nawatakia kila la kheri katika mechi ya fainali waibuke na kombe na watupe raha ambayo Watanzania tumeikosa kwa muda mrefu.”

Akijibu Kikwete, Jussa alihoji, “wakupe raha wakati wewe uliwapa karaha kwa kuifisidi Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa kuyapindua maamuzi ya Wazanzibari na kuyavuruga maridhiano yao?”

Akaongeza, “Ati anzibar Heroes wakutoe kimasomaso. Wanachofanya Zanzibar Heroes ni kuwatusi wote walio na hasadi na Zanzibar yao.”

Akijaribu kumtetea Kikwete, mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alimtaka Jussa kupunguza hasira.

Akiandika katika ukusa wake wa twitter mara baada ya Jussa kushushia kombora Kikwete, Zitto aliandika: Jussa.

Naye Jussa akijibu Zitto aliandika: Naam! Zitto akaongeza, “please.” Jussa akauliza: “What? Akasema, “mimi sijazoea kuwa na ndimi mbili.”

Zitto ambaye amekuwa akitajwa kuwa alikuwa na uswahiba wa karibu na Kikwete, safari hii alijibu maandishi ya Jussa katika kile kinachoonekana kuogopa kushambuliwa alisema, “acha tufurahi na mpira bwana….”

Jussa akasema, “of course (ni sawa), tunafurahi na mpira. Lakini hilo halifuti tuliotendewa na tunayoendelea kutendewa.”

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wajuu wa CUF kumtuhumu hadharani na kwa maneno makali Kikwete, kuwa ndiye aliyeagiza kupinduliwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Uchaguzi mkuu huru na haki wa rais, wawakilishi na madiwani, ulifanyika tarehe 25 Oktoba 2015, Visiwani.

Ulifutwa na Jecha Salim Jecha, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kwa kile kinachoitwa na waangalizi wa ndani na nje, “kuhalalisha uporaji wa ushidi wa mgombea wa upinzani, Maalim Seif Shariff Hamad.”

Jecha alisema, ameamua kuufuta uchaguzi huo na matokeo yake, kufuatia madai ya kutawaliwa na hila, mizengwe na kugubikwa na udanganyifu.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na wangalizi wa uchaguzi huo kutoka ndani na nje zilisema, “uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika 25 Oktoba 2015, ulikwenda vizuri na kuwapa nafasi wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.”

Inasema, “zoezi la upigaji kura lilimalizika vema. Kazi ya kuhesabu kura nayo ilikwenda vizuri na fomu za matokeo ya uchaguzi kwa kila kituo cha kupigia kura zilikamilika.

“Kazi ya majumuisho ya kura katika ngazi ya majimbo nayo ilikwenda vizuri na kukamilishwa bila ya kuwepo malalamiko yoyote kutoka chama chochote kilichokuwa kinashiriki uchaguzi huo.

“Ni kutokana na kukamilika kwa hatua zote hizo bila ya kuwepo malalamiko yoyote, na kwa kufuata masharti ya kifungu cha 88 cha Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Na. 11 ya 1984, ndipo Wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo yote ya Unguja na Pemba wakawatangaza washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani na pia kuwapa taarifa za maandishi wagombea walioshinda.

“Taarifa inasema, majumuisho ya kura za urais yalishakamilika katika majimbo yote 54 na matokeo ya kila jimbokubandikwa nje ya vituo vya majumuisho baada ya kukamilisha masharti ya kifungu cha 42(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Aidha, baadhi ya nchi rafiki na Tanzania ikiwamo Marekani, Uingereza, Umoja wa Ulaya (EU) na jumuiya za kimataifa na kikanda, pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zimetaka mgogoro wa kisiasa Visiwani upatiwe ufumbuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!