Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Juma Duni Haji aikosoa SMZ
Habari za Siasa

Juma Duni Haji aikosoa SMZ

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimedai kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ina tabia ya kutenga bajeti isiyokidhi mahitaji pia kukopa kwa masharti magumu na riba kubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni visiwani Zanzibar, Naibu Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji amesema Sh. 400 Bilioni zilizotengwa katika mwaka wa fedha wa 2019/20, hazikidhi mahitaji ya kiuchumi na ustawi wa jamii ya visiwa hivyo.

Duni ameeleza kuwa, Visiwa vya Zanzibar vina changamoto nyingi hususan katika sekta ya afya, elimu, miundombinu na maji.

“Nimeelezwa kwamba, bajeti hiyo itakuwa na nakisi ndogo ya 400 Bilioni, kwa kweli bajeti hii ni ndogo sana ukilinganisha na mahitaji ya kiuchumi na ustawi wa jamii ya Zanzibar,” amesema Duni.

Wakati huo huo, Duni amesema kitendo cha SMZ kukopa madeni yenye riba kubwa na masharti magumu, kimepelekea serikali hiyo kuwa na malimbikizo ya madeni ya ndani na nje ya nchi.

Amesema, hadi sasa Zanzibar inadaiwa Sh. 815.9 Bilioni, huku deni la nje likiwa ni Sh. 678.4 Bilioni na kwamba, SMZ imeshindwa kulipa kwa wakati malimbikizo ya viinua mgongo vya wastaafu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!