Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jukwaa la Katiba ‘wajivisha mabomu’ kwa Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Jukwaa la Katiba ‘wajivisha mabomu’ kwa Rais Magufuli

Deus Kibamba, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (kulia) anayefuata ni Hebron Mwakagenda, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukata. Picha ndogo Rais John Magufuli
Spread the love

JUKWAA la Katiba Tanzania wamempa Rais Dk. John Magufuli kwa kumtaka ajiandae kupokea maandamano ya amani kwa ajili ya kumpongeza pamoja na kumtaka afufue mchakato wa katiba mpya, anaandika Dany Tibason.

Mwenyekiti wa bodi ya Jukwaa hilo, Hebron Mwakagenda amesema wadau wa masuala ya katiba wameazimia kufanya mambo mbalimbali.

Amesema wadau wa Jukwaa la Katiba wamependekeza kufanya maandamano ya amani nchi nzima 30 Oktoba mwaka huu na wanatarajia Rais Magufuli atayapokea.

Mwakagenda amesema maandamano hayo yanalenga kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi yake ya kupambana na ufisadi na ubadhilifu wa mali ya umma pamoja na kurejesha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.

Mwenyekiti huyo amesema katika maandamano hayo kutapatikana fursa ya kuonana uso kwa uso na mkuu wa nchi ili kumweleza wazi kuwa Watanzania wana kiu ya kuwa na katiba mpya ambayo inajibu matakwa yao.

Amesema Rais ataelezwa wazi kuwa katiba ambayo wananchi wanaitaka ni katiba itakayotokana na maoni ya wananchi ambayo yalikusanywa na tume ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba.

“Sisi kama Jukwaa la katiba Tanzania tumemwandikia barua zaidi ya nne Rais Magufuli, lakini hatujapata majibu sasa hatujui kama hizo barua kazipata kanyamaza au la.

“Lengo kubwa ni Rais kufufua mchakato wa katiba kwa kuwa fedha nyingi za walipa kodi zaidi ya Sh. bilioni 100 zimetumika,lakini katiba ya wananchi haijapatikana jambo ambalo ni fedheha kwa watanzania.

“Kwa maana hiyo basi tukiweza kukaa meza moja naye tutaongelea umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya na tumaamini atatuelewa na kama atafanya hivyo atakuwa ameshusha kiu ya Watanzania wengi wanaotaka kuona katiba mpya ikifanya kazi” amesema Mwakagenda.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jukwaa hilo kutoka Tanzania Bara na Visiwani wameridhia kufanya maandamano hayo mwishoni mwa mwezi ujao kutokana na jitihada zao za kutaka kuonana na Rais kukwama licha ya kumuandikia barua zaidi ya mara nne kwa lengo la kuonana naye kwa ajili ya kufanya mazungumzo juu ya suala hilo.

Akizindua Bunge Novemba mwaka jana Rais Magufuli alisema kuwa serikali imepokea kiporo cha mchakato wa katiba mpya ambao haukukamilika awamu iliyopita kutokana na kuchelewa kuandikisha wapiga kura, lakini mwishoni mwa mwaka jana wakati wa mkutano wake na wanahabari Rais Magufuli alisema kuwa suala la Katiba mpya sio kipaumbele chake.

Mchakato wa Katiba mpya ulioanza mwaka 2011 ulisimamiwa vyema na iliyokuwa Tume ya Marekebisho ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Katika mchakato huo waliandaa rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete Desemba mwaka 2013.

Wakati wa uwasilishwaji wa rasimu hiyo kwenye Bunge Maalumu la Katiba wajumbe wa upinzani zaidi ya 200 waliounda Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) walisusia vikao hivyo kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa chombo hicho ikiwamo kutozingatia maoni ya wananchi yalikuwa kwenye rasimu ya Katiba ya jaji Warioba.

Hata hivyo kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani nchini kuulalamikia mhimili wa serikali kuingilia mhimili wa Bunge na hivyo kuufanya kukosa uhuru na kusababisha kuminywa kwa demokrasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wagombea 127 wa udiwani kutoka vyama 18 kuchaguliwa kesho

Spread the loveWagombea udiwani 127 kutoka vyama 18 vya siasa wanatarajiwa kupigiwa...

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

error: Content is protected !!