Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: TAG jiengeni viwanda
Habari za Siasa

Rais Magufuli: TAG jiengeni viwanda

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli ameshauri Kanisa la Assembly of God (TAG), kuelekenza nguvu katika ujenzi wa viwanda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma leo tarehe 14 Agosti 2020, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 13 ya Moto katika Mkutano Mkuu wa kanisa hilo.

Ni baada ya kanisa hilo kueleza, kwamba limetenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu.

“Nataka nikuhakikishie Askofu Mkuu tuko pamoja katika hilo, na mimi nafikiri sio tu kujenga Chuo Kikuu lakini mnaweza kutenga eneo kwa ajili ya kujenga viwanda.

“Hata kama ungeanzisha kiwanda cha kuchimba chuma kule Manda ili sisi Tanzania tusiwe tunaagiza chuma kutoka kule nje. Tuchimbe chuma yetu ambayo ni first class (Daraja la Kwanza)..halafu na madini mbalimbali na viwanda vile vikawa chini ya TAG,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, nafasi ya kuanzisha viwanda katika serikali yake bado hipo “kwa hiyo Baba Askofu Mkuu na ndugu wachungaji na maaskofu wote, chumba hicho bado kipo wazi.

“…na mimi napenda kuwathibitishia kabisa kwasababu tunaijenga Tanzania ya viwanda, mimi na serikali yangu kama tupo, tutaendelea kuwasapoti kwa nguvu zote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!