Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Sijamtuma mtu akagombee, awapa ujumbe wanaCCM
Habari za SiasaTangulizi

JPM: Sijamtuma mtu akagombee, awapa ujumbe wanaCCM

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amewatahadharisha wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaohusika na uteuzi wa wagombea wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, kuwa makini na makada wanaotumia majina ya viongozi kuomba kupitishwa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo Alhamisi Julai 16, 2020 wakati Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua wakiwemo wakuu, wilaya na katibu tawala.

Rais Magufulu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM ametoa kauli hiyo kipindi ambacho chama hicho kiko katika mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu kuomba kuteuliwa kuwania udiwani, ubunge na uwakilishi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Paul Makonda, Mtia nia jimbo la Kigamboni

Mchakato huo umeanza tarehe 14 na utahitimsihwa tarehe 17 Julai 2020.

Rais Magufuli amesema, hakuna mtu yoyote aliyemtuma kwenda kugombea katika uchaguzi huo.

Amesema watu watakaosema wametumwa kugombea na viongozi wa ngazi za juu wa serikali, akiwemo yeye ni waongo hivyo wapuuzwe.

Rais Magufuli amesema, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu Mweyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula wala viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, hawajawatuma watu kwenda kugombea.

Soma zaidi hapa

Ubunge CCM: ‘Wateule wa Rais’ wachongewa , CDF na Samia watoa neno

“Nataka kuwathibitishia hakuna mtu yeyote aliyetumwa na mimi wala makamo wa rais, hakuna mtu aliyetumwa na waziri mkuu, Mzee Mangula, wala Katibu Mkuu Dk. Bashiru (Ally). Kwa hiyo kama wapo watu wanazungumza nimewatuma ni waongo,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, ujumbe huo uwafikie watu wote, wenye dhamira ya kuomba kupitishwa na CCM kugombea katika uchaguzi huo, kupitia majina ya viongozi, pamoja na WanaCCM wote.

Mwenyekiti huyo wa CCM amewataka wanaohusika na masuala ya uteuzi wa wagombea, wawateue wagombea kulingana na sifa zao na ushawishi wao kwa wananchi.

Soma zaidi hapa

JPM atengua Ma-DC, RAS, DED na RC akiwemo Makonda

“Huu ujumbe uwafikie WanaCCM wote, wapime wagomeba kulingana na ninyi mnavyoona watawafaa kwenye uwakilishi, siwezi nikatuma mtu wote wako sawa. Muwapime kisawasawa, sababu nimesikia kila mahali mimi nimetuma watu,” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo wa nchi amesema, kama angetaka kumtuma mtu, angetangaza mwenyewe au kuwateua kupitia ubunge wa kuteuliwa na rais.

Kitila Mkumbo, mtia nia jimbo la Ubungo (Ccm)

“Kama ningesubiri kutuma, si ningekaa ningesubiri viti vyangu 10 vya kuteua, nataka muwatume ninyi Watanzania na wala hawajatumwa na vyombo vya ulinzi na usalama, kama kiongozi angekutuma angekuteu, tukazingatie maandili yetu,” amesisitiza Rais Magufuli.

Hii ni zaidi ya mara mbili kwa Rais Magufuli kuwaonya wenye tamaa ya madaraka, ambapo aliwaonya wateule wake, kutoachia madaraka yao kwa ajili ya kujitosa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, na kuwataka waridhike na nafasi zao.

Pia, Rais Magufuli amesema, kwa taarifa alizonazo hadi leo Alhamisi alfajiri, waliojitokeza kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa majimbo, viti maalum na wawakilishi kupitia CCM ni 8,205.

Amesema, kati ya hao, Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na wagombea 829, Arusha 320, Kusini Unguja 53 na Kagera 328.

Rais Magufuli amesema, wagombea wa majimbo wako 6,833, viti maalum 1,539 na wawakilishi 133.

 

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!