Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko JPM: Shukrani ya punda, mateke
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

JPM: Shukrani ya punda, mateke

Rais John Magufuli, mgomba Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM
Spread the love

DAKTARI John Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, licha ya kufanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo Tanzania, bado kuna watu wanamtukana. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Septemba 2020, akiwa kwenye eneo la Myakato, jijini Mwanza ambapo kesho tarehe 7 Septemba 2020, anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa CCM Kirumba.

“Nimewaletea ndege, nimewaletea vivuko lakini kuna watu wanapanda na wakishuka tu, wananitukana. Kweli shukurani ya punda ni mateke,” amesema Dk. Magufuli.

Akiwa katika eneo la Magu jijini humo Dk. Magufuli amesema, anastahili kuongezewa miaka mitano ili kukamilisha miradi yake aliyoianzisha.

Amesema, katika utawala wake wa miaka mitano (2015 – 2020), amefanya miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo reli ya kisasa na kwamba, wananchi wasipompa kura na kuwapa wengine, hawatoendeleza miradi hiyo na badala yake watakula tu.

“Ndio maana nawaomba ndugu zangu, mnipe tena miaka mitano, mkiacha kunipa miaka mitano, hiyo reli atakuja kujenga nani?

“Watakuja wengine, watakuja kula tu.  Mbona hawakujenga miaka 40 iliyopita? ndani ya miaka mitano tumeanza kujenga. Wana Magu nipeni tena miaka mitano, na mimi naona ninastahili kupewa miaka mingine mitano,” amesema Dk. Magufuli.

Akifafanua maendeleo ya reli hiyo Dk. Magufuli amesema, tayari reli hiyo imeanza kujenga na imefikia hatua nzuri.

“Tumeanza kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, tumeishatengeneza kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro na kwa wale mnaokwenda Dar es Salaam mseme kwa sababu mimi sisemagi uongo.

“Sasa tunatengeneza kutoka Morogoro – Mkutupora mpaka Dodoma. Wiki iliyopita tumetangaza tenda ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza kupitia Shinyanga hadi Isaka kwa kilometa 250,” amesema.

Amesema, hakuna aliyetarajia kuwa kama Tanzania tutakuwa na treni ya umeme, na kuwa terni hizo zilikuwa zikishuhudiwa katika nchi za Ulaya.

Dk. Magufuli awali alipokuwa katika eneo la Igoma, akielekea Mwanza mjini amesema, ana mpango wa kuinganisha Igoma, Kiseas na Isiri kuwa wilaya moja.

Amesema, kwa eneo hilo kulifanya wilaya, itakuwa na bajeti yake “nataka Igoma, Kisesa na Isiri niitengeneze wilaya moja. Bajeti itaongeezeka na jiji litaipangiwa fedha nyingi na hivyo kuwa na maendeleo zaidi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

error: Content is protected !!