
Balozi Job Lusinde
DAKTARI John Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesikitishwa na kifo cha Balozi Job Lusinde, aliyekuwa mdhamini wa chama hicho katika uasisi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Lusinde ambaye alikuwa miongoni mwa mawaziri 11 wa kwanza wa Serikali ya Tanganyika, amefariki dunia alfajiri ya tarehe 7 Julai 2020.
Leo tarehe 8 Julai na Rais John Magufuli, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameomb0leza kifo cha Balozi Lusinde, akisema kwamba atakumbuka mchango wake mkubwa alioutoa kwa taifa.
Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde. Nawapa pole Familia, wana Dodoma na Watanzania. Nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee wa Dodoma. Pumzika salama Mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri.
— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) July 8, 2020
“Nimesikitishgwa na kifo cha Mzee wetu Balozi Job Lusinde. Nawapa pole familia, wana Dodoma na Watanzania. Nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa taifa akiwa waziri, balozi, mdhamini wa CCM na kiongozi wa Wazee wa Dodoma. Pumzika salama mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri,” ameombolewa Rais Magufuli.
Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, chama hicho kinamlilia Balozi Lusinde, kwa kuwa alikuwa sehemu ya waasisi wake.
“Chama kinamlilia Mzee wetu Job Lusinde, sehemu ya waasisi wetu, kiongozi katika chama na serikali, mzee na mshauri wetu wa chama kutoka Jiji la Dodoma.
“Mzee Lusinde alikuwa mjumbe wa Baraza la Wadhamini la CCM. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe,” ameandika Polepole katika ukurasa wake wa Twitter.
Chama @ccm_tanzania kinamlilia Mzee wetu Job Lusinde, sehemu ya waasisi wetu, Kiongozi katika Chama na Serikali, Mzee na Mshauri wetu wa Chama kutoka Jiji la Dodoma. Mzee Lusinde alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la CCM. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe. pic.twitter.com/5fkB4HROfL
— Humphrey Polepole (@hpolepole) July 8, 2020
More Stories
Silinde atembelea shule ya King’ongo-Ubungo, atoa maagizo
Aliyekuwa mgombea udiwani NCCR-Mageuzi atimkia Chadema
Majaliwa amkabidhi binti mwenye ulemavu nyumba, milioni 18