Moja ya ndege za Bombadier inayomilikiwa na Tanzania

JPM: Ndege iliyoshikwa Canada, inakuja

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bombardier Q400, iliyoshikiliwa nchini Canada, imeachwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akishiriki kwenye Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCMTaifa, Rais Magufuli amesema, ikianza safari ya kurejea nchini, mamlaka itatangaza na itapokelewa jijini Mwanza.

“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza,” Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti CCM Taifa, ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Desemba 2019.

Tarehe 23 Novemba 2019, mamlaka nchini Canada zilikamata ndege hiyo ilizuiwa kwa amri ya mahakama. Ilikuwa mara ya pili kwa ndege ya Tanzania kuzuiliwa nchini Canada.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi alieleza, sababu ya kukamatwa kwa ndege hiyo, ni kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia, Hermanus Steyn.

Steyn pia alifungua kesi nchini Afrika Kusini Agust iliyosababisha ndege aina ya Air Bus 220-300 izuiliwe.

RAIS John Magufuli amesema, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bombardier Q400, iliyoshikiliwa nchini Canada, imeachwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). Akishiriki kwenye Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Magufuli amesema, ikianza safari ya kurejea nchini, mamlaka itatangaza na itapokelewa jijini Mwanza. “Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza,” Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti CCM Taifa, ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Desemba 2019. Tarehe 23 Novemba 2019, mamlaka nchini Canada zilikamata ndege hiyo ilizuiwa kwa amri ya mahakama. Ilikuwa mara ya pili kwa ndege ya Tanzania…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!