Rais John Magufuli

JPM: Mungu kajibu maombi 

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, Mungu amejibu maombi ya Watanzania kuepusha ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virisi vya corona (COVID-19) nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea). 

Akihudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata Dodoma leo tarehe 7 Julai 2020, Rais Magufuli amesema Mungu amesikia na kupokea sala za Watanzania kuhusu kuepusha janga la corona.

“Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake maambukizi ya corona yamepungua na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa corona ingesababisha madhara makubwa,” amesema Rais Magufuli.

Pia amewashukuru viongozi wa dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu aepushe janga hilo.

Kwenye kanisa hilo, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha zaidi ya Mil 17, katika fedha hizo, yeye ametoa kiasi cha Sh. 10 milioni na mifuko 76 ya saruji.
RAIS John Magufuli amesema, Mungu amejibu maombi ya Watanzania kuepusha ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virisi vya corona (COVID-19) nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).  Akihudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata Dodoma leo tarehe 7 Julai 2020, Rais Magufuli amesema Mungu amesikia na kupokea sala za Watanzania kuhusu kuepusha janga la corona. https://www.youtube.com/watch?v=BZjibTXNijU “Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake maambukizi ya corona yamepungua na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa corona ingesababisha madhara makubwa,” amesema Rais Magufuli. Pia amewashukuru…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!