Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM awatumbua RC Gambo, DC na DED Arusha
Habari za Siasa

JPM awatumbua RC Gambo, DC na DED Arusha

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa viongozi watatu wa Mkoa wa Arusha na kufanya uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa leo Ijumaa usiku tarehe 19 Juni 2020 imeelezea mabadiliko hayo.

Kwanza, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na amemteua Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Kimanta alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.

Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli itajazwa baadaye.

Pili, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha(DC), Gabriel Daqarro na amemteua, Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Kihongosi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa.

Tatu, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha (DED) Dk. Maulid Madeni na amemteua Dk. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Dk.Pima alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Aidha, Rais Magufuli amemteua, Jerry Mwaga kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Kabla ya uteuzi huo, Mwaga alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Jumatatu tarehe 22 Juni, 2020 saa 2:30 asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!