Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM awachimba mkwara wahujumu uchumi walioukataa msamaha wake
Habari za SiasaTangulizi

JPM awachimba mkwara wahujumu uchumi walioukataa msamaha wake

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amewapa angalizo watuhumiwa wa uhujumu uchumi, walioshindwa kutumia fursa ya msamaha alioutoa hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Septemba 2019, Rais Magufuli amesema baadhi ya watuhumiwa wamesita kuomba msamaha, wakidanganywa kwamba msamaha wake ni uongo.

Rais Magufuli ameeleza kuwa, kama washtakiwa hao watachagua kusikiliza watu wanaowashauri wasiombe toba, wakiendelea kukaa gerezani wasimlaumu mtu yeyote.

 “Ninafahamu wako wanaodanganywa wanaambiwa huu msamaha ni wa uongo.  Huwa hakuna msamaha  wa uongo, ukishatoa msamaha umetoa, huwezi ukatoa msamaha wa majaribio. Huwezi ukatoa msamaha wa kumtega mtu. Msamaha ukishatoa ni msamaha, msamaha ni lazima uwe,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

 “Hao wanaowadanganya wanataka waendelee kukaa gerezani, na kadri watakavyokaa gerezani wasimlaumu yeyote. Ninafahamu wapo wengine wanadanganywa na mawakili wao, ili kusudi wawachomoe pesa.

Kwamba wakiomba msamaha watakua wamejishtaki wenyewe, wachague kusikiliza mawakili wao au wewe DPP au ushauri niliotoa. Ndio maana nimetoa siku saba, zikiisha sitatoa tena.”

Aidha, Rais Magufuli amesema msamaha huo hauwahusu watuhumiwa wa uhujumu uchumi, watakaoleta maombi yao baada ya muda wa msamaha kufika kikomo.

“Nitoe angalizo DPP,  kwa wale wanaoshikwa na kesi za uhujumu uchumi kuanzia leo usifikiri wanahusika na msamaha huu. Kashughulike nao kisawa sawa. Lakini nitoe tahadhari, baada ya siku hizi wale wote watakaoshikwa kwenye masuala ya uhujumu uchumi sheria ichukue mkondo wake,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema hatua ya mamlaka husika kuwapa msamaha watuhumiwa hao, haimaanishi kwamba kesi za uhujumu uchumi zimefutwa, bali zitaendelea kuwepo kwa mujibu wa sheria.

“Isije ikawa imejengeka mazoea kwamba kesi ya uhujumu uchumi haipo. Sio kwamba kesi za uhujumu uchumi nimezifuta. Zile ziliundwa kwa mujibu wa sheria, ila kwenye hili  nilitoa ombi na inaonekana lilikubalika kwako na wasaidizi wako, na mtu mwenye mamlaka ya kufuta kesi ni DPP pamoja na mahakama,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“Watakaoshikwa baada ya siku hizi nilizoongezea na wale wa kesi mpya,  sababu kuna kesi leo mtu akihujumu wapelekwe kwenye kesi za uhujumu uchumi hawahusiki na msamaha, watakaoshikwa leo kesho na kadhalika, waendelee na kesi zao, hizi siku saba ni kwa wale walioomba msamaha.”

Rais Magufuli ameongeza muda wa siku saba, kwa watuhumiwa ambao barua zao za maombi ya msamaha hazijamfikia DPP Mganga kutokana na sababu mbalimbali, maombi yao yasikilizwe.

“Kama kweli wako waliokwamishwa na wamekwama kutokana na umbali kutoka mikoani hadi hapa na wengine kwenye mchakato ndani ya magereza, umeniomba siku tatu sio. Mimi naona nikupe siku 7 ili usije ukaniomba siku nyingine. Nina uhakika hawatarudia makosa yao, nafikiri niwaongezee siku saba zaidi, “ amesema Rais Magufuli.

Kuhusu watuhumiwa wa uhujumu uchumi 467 walioandika barua za kuomba msamaha, Rais Magufuli amemtaka Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kukamilisha haraka mchakato wa kisheria, ili wahusika waachwe huru.

“Ningeomba ofisi ya DPP muharakishe hatua,  watu waanze kutoka wakajumuike na familia zao, mtu akishalipa hizo hela na mkisahafanya hizo hatua za mahakama, muwafikishe haraka kwenye vyombo vya sheria ili waanze kuachiwa wakajumuike na familia zao,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!