‘JPM atumie Busara’

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

 

BARAZA la Maaskofu Tanzania (TEC) limemtaka Rais John Magufuli kutumia busara katika hatua mbalimbali za kupambana na ufisadi, anaandika Wolfram Mwalongo.

Kauli hiyo imetolewa jana mbele ya wanahabari na Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi Jimbo Katoriki la Bukoba alipokuwa jijini Mwanza  kwenye kongamano la tatu la taifa la Ekaristi Takatifu linalotarajiwa kufanyika tarehe 10 Juni mwaka huu.

Kilaini ameseama rais ili afanikiwe lazima tuungane kumwombea iliafanye maamzi sahihi na wananchi kumunga mkono ili kutokomeza uhalifu na ufisadi nchini.

Aidha amesema kuwa taifa lipo katika hofu kubwa hasa kutokana na mauaji ya watu  yaliyotokea siku za karibuni Mwanza na Tanga kutokana na watu kutokuwa na hofu ya mungu.

Kongamano hilo litakuwa na maombi maalumu kwa ajili ya kuombea viongozi pamoja na familia ili kudumisha upendo na amani.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
  BARAZA la Maaskofu Tanzania (TEC) limemtaka Rais John Magufuli kutumia busara katika hatua mbalimbali za kupambana na ufisadi, anaandika Wolfram Mwalongo. Kauli hiyo imetolewa jana mbele ya wanahabari na Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi Jimbo Katoriki la Bukoba alipokuwa jijini Mwanza  kwenye kongamano la tatu la taifa la Ekaristi Takatifu linalotarajiwa kufanyika tarehe 10 Juni mwaka huu. Kilaini ameseama rais ili afanikiwe lazima tuungane kumwombea iliafanye maamzi sahihi na wananchi kumunga mkono ili kutokomeza uhalifu na ufisadi nchini. Aidha amesema kuwa taifa lipo katika hofu kubwa hasa kutokana na mauaji ya watu  yaliyotokea siku za karibuni Mwanza na Tanga kutokana na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Masalu Erasto

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube