Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko JPM atuma salamu za rambirambi vifo vya watu 19 Songwe
Habari Mchanganyiko

JPM atuma salamu za rambirambi vifo vya watu 19 Songwe

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali ya barabara iliyotokea wilayani Mbozi mkoa wa Songwe jana tarehe 21 Februari 2019.Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Songwe , Brigedia Jenerali,Mstaafu, Nicodemas Mwangela kufikisha salamu zake zza pole kwa familia hizo.

Aidha, Rais Magufuli amezitaka mamlaka zinazohusika na usalama wa barabarani mkoani Songwe kufanya uchunguzi wa ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili pamoja na kujipanga vizuri kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu na robo usiku katika mteremko wa Senjele ambapo Lori lililokuwa linatokea Tunduma kwenda Mbeya Mjini liligonga basi la abiria kwa nyuma, kisha basi hilo na kusababisha vifo vya watu 19.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametoa mkono wa pole kwa familia ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye amefiwa na mtoto wake, Zul Hamis Kigwangalla jana tarehe 21 Februari 2019.

“Rais Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wamefika nyumbani kwa familia hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam na kukutana na baadhi ya wanafamilia wakiongozwa na mama wa marhemu, Dk. Bayoum Kigwangalla wakiwa katika maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Nzega mkoani Tabora,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!