Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM atema nyongo, asema ‘sitoacha kutumbua’
Habari za SiasaTangulizi

JPM atema nyongo, asema ‘sitoacha kutumbua’

Rais John Magufuli
Spread the love

SIKU moja baada ya kufanya mabadiliko madogo serikalini, Rais John Magufuli amesema kuwa, hatokoma kuteua viongozi wapya na au kutengua uteuzi wa viongozi wanaokwenda kinyume na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Rais Magufuli ametoa msimamo huo leo tarehe 9 Januari 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha viongozi wapya aliowateua jana, akisema kuwa hatoacha ‘kutumbua’ hata kama mhusika ni rafiki yake.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uapisho, Rais Magufuli ameeleza changamoto mbalimbali zinazoikabili serikali yake, hasa katika wizara ya madini na serikali za mitaa, zilizompelekea kufanya mabadiliko hayo.

“…Wameona Tanzania ni eneo la watu ambao hawajitambui, tunawataalamu, wahandisi na majiolojia lakini ‘they are just sleeping’ (wamelala), mimi nitanendelea kufanya mabadiliko na kila ninapoona mahali haparidhishi nitaondoa watu hata Biteko nikio siridhishwi utaondoaka, huu ndio ukweli sababu tunahitaji pesa, tunahitaji rasilimali za Watanzania zinufaishe wananchi wetu,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu wizara ya madini, Rais Magufuli ameonesha kukerwa na kitendo cha wizara hiyo kutotekeleza ipasavyo sheria mpya ya madini na kupelekea serikali kupoteza mapato hasa kupitia madini ya dhahabu.

“Wizara ya madini kuna changamoto kubwa, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki nchi inayoongoza kwa kuuza dhahabu sio Tanzania , ukishaona ripoti kama hii wakati Tanzania tunajua tunaongoza kwa kuwa na dhahabu nyingi lazima tuangalie wapi tulipokosea. Sheria imepitishwa ni lazima tuangalie udhaifu uko wapi,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.

“Na udhaifu huu wizara ya madini haiwezi ikaukwepa sababu sheria ipo, na kila siku tunahimiza wananchi wachukue maeneo, tumeshajiuliza zile dhahabu zinazochimbwa zinauzwa wapi, tumeshajiuliza sisi wizara ya madini kujua yanayochimbwa yanauzwa wapi, na wanakouza inabidi kuuliza sisi tunapata fedha kiasi gani, hilo ni suala la wizara haikuwa kazi ya bunge au waziri au rais kuuliza, wizara ina waziri makamishna na watendaji wa kila aina.”

Rais Magufuli amesema kuwa “Sheria ya madini imeweka wazi namna ya kushiriki na kuingia mkataba na nchi nyingine na makampuni makubwa, na ushiriki wa wachimbaji wadogo, nina uhakika kwenye sheria hii kuna mahali inaagiza uanzishwaji wa mineral center, je zimeanzishwa ngapi , ziko wapi, sababu tungekuwa na mineral center dhahabu ingeenda kuuzwa pale, tungekuwa na taarifa hata za kila wiki, tungejua kwamba leo dhahabu kiasi hiki imeingizwa katika center na serikali imepata kiasi hiki.”

Kufuatia changamoto hizo, Rais Magufuli amesema amempandisha cheo Dotto Biteko kutoka unaibu waziri wa madini hadi kuwa waziri kamili, kwa kuwa ana imani ataitendea haki nafasi hiyo kutokana na uzoefu aliokuwa nao kuhusu sekta ya madini.

“Niwapongeze jinsi bunge na mahakama mnavyofanya kazi, mhimili hii miwili imesaidia serikali kufanya kazi, mfano wewe spika (Job Ndugai) katika bunge lako huwa unateua kamati, kwenye kamati ya madini ulimteua Biteko, nimeona jinsi alivyokuwa anaichachafya serikali, michango yake katika ushauri wa serikali, na ilipokuja suala la madini uliunda kamati ya kuchunguza madini yanavyoibiwa,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.

“Na mmoja kati ya wanakamati ulimteua Biteko, ndio maana kamati ilipomaliza kuchukua ripoti tukamchukua serikalini kuwa naibu waziri baada ya kufanya kazi vizuri, tukasema basi huyo aliyeundwa na kuwa mwenyekiti wa kamati maalum ya kuchunguza madini, na sisi tukaona tumchague kwa hiyo ni wewe spika umetupa mwelekeo wa kumchagua.”

Kufuatia mabadiliko hayo kwenye wizara ya madini, Rais Magufuli amemuiagiza Biteko na watendaji wa wizara hiyo, kutekeleza ipasavyo sheria mpya ya madini ikiwemo kuanzisha vituo vya uuzaji madini ‘Mineral Center’.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameeleza sababu za kufanya mabadiliko katika wizara ya afya kwa kumhamisha katibu mkuu wake ambapo alimteua Zainab Chaula aliyetoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kushika wadhifa huo akisema kuwa mgogoro wa waziri wa wizara hiyo Ummy Mwalimu na Chaula umpelekea kuwakutanisha pamoja.

“Nilikuwa nasoma sms ya waziri wa afya na naibu katibu wa TAMISEMI kuhusu ujenzi wa afya wanashindiliana , nikasema hawa ili niwakomeshe niwaweke wizara moja. Kuna sms za huyu dada yake, nikasema akakae na dada yake kwenye wizara moja akagombane nae kweli kweli.Katika kazi hizi kuna challenge (changamoto) nyingi, nina fahamu halmashauri watu wanavyogombana,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!