Rais John Magufuli amekabidhiwa tuzo ya heshima na Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Barnabas Mtokambali

JPM apewa tunzo ‘udhibiti corona’

Spread the love

RAIS John Magufuli amekabidhiwa tuzo ya ‘hongera’ kutokana na namna alivyokabiliana na ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tuzo hiyo imetolewa na Kanisa la Assembly of God jijini Dodoma leo tarehe 14 Agosti 2020, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 13 ya Moto katika Mkutano Mkuu wa kanisa hilo.

Akikabidhi tuzi hiyo, Askofu Mkuu wa TAG, Barnabas Mtokambali amesema, tuzo hiyo imetolewa na Baraza pia Mkutano Mkuu wa kanisa hilo katika kikao chake kilichofanyika kwa siku 13.

“Baraza kwa pamoja lilitoa uamuzi kwamba, tuzo maalum ya heshima ya Baraza Kuu la Tanzania Assemblies of God (TAG) itolewe kwako wewe muheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua jinsi ulivyoliongoa Taifa letu kumtegemea Mungu katika kipindizi kigumu cha janga la corona.

“Wakati mataifa mengine yaliweka nguvu kwenye kuwazuia watu wao wasitoke majumbani na kufunga shughuli mbalimbali za kuletea mataifa yao maendeleo, wewe umefanya jambo tofauti kabisa duniani. Ulilielekeza Taifa kufunga na kuomba kwa siku tatu mfululizo,” amesema Askofu Mtokambali.

Amesema, baada ya maombi hayo, Rais Magufuli alisimama tenda mbele ya Watanzania na kutangaza kwamba sasa tumshukuru Mungu kwa kuwa amepokea maombi yetu.

Askofu Mtokambali amesema, uamuzi wa Rais Magufuli kutofungia wananchi ndani wakati wa janga la corona, na kuelekeza katika kumtegemea Mungu, ameliweka taifa kwenye nafasi ya kipekee.

Amesema “aidha uamuzi wako wa kutowafungia watu nyumbani na badala yake kuwaelekeza wafanye kazi na wamtafute Mungu wao kwa bidi ambaye ndio jawabu la kweli la mambo yote, Mheshimiwa Rais umeliweka taifa letu kwenye nafasi ya kipekee sana sana duniani.

“Katika kumtegemea Mungu kwenye medani za kiroho na pia kuliwezesha Taifa kutoyumba kiuchumi, jambo hili limegusa sana baraza hili. Tunamuomba Mungu akubariki sana sana kwa kumtanguliza yeye katika uongozi wa taifa letu.”

RAIS John Magufuli amekabidhiwa tuzo ya ‘hongera’ kutokana na namna alivyokabiliana na ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Tuzo hiyo imetolewa na Kanisa la Assembly of God jijini Dodoma leo tarehe 14 Agosti 2020, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 13 ya Moto katika Mkutano Mkuu wa kanisa hilo. Akikabidhi tuzi hiyo, Askofu Mkuu wa TAG, Barnabas Mtokambali amesema, tuzo hiyo imetolewa na Baraza pia Mkutano Mkuu wa kanisa hilo katika kikao chake kilichofanyika kwa siku 13. “Baraza kwa pamoja lilitoa uamuzi kwamba, tuzo maalum ya heshima ya Baraza Kuu…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!