Friday , 29 March 2024
Habari za SiasaTangulizi

JPM amkubali Sugu

Spread the love

RAIS John Magufuli, amemrudisha jukwaani Joseph Mbilini (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini kumalizia hotuba yake licha ya kuondolewa na msimamizi wa shughuli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakati akizungumza malalamiko ya wananchi wa Mbeya leo tarehe 26 Aprili 2019 mbele ya Rais Magufuli aliyepo jijini humo kwa ziara ya siku nane, mara kadhaa Sugu alikatizwa akiambiwa, muda wake umekwisha.

Hata hivyo, Sugu aliendelea kuhutubia jambo ambalo lilisababisha kuondolewa ‘kwa lazima’ huku akizungumza.

Rais Magufuli aliingilia kati na kutaka arudishwe jukwaani amalizie hotuba yake. Rais Magufuli alisema “haya malizia sekunde,” hatua ambayo ilimpa nafasi Sugu kurejea na kumalizia hotuba yake.

Kabla ya kuondolewa jukwaani, Sugu alitonesha donda kwa kueleza kuwepo kwa ‘ubaguzi’ wa kivyama kwamba, wafuasi wa Chadema walisukumwa nyuma ya wengine (hakutaja chama).

“Naona kuna mgawanyiko hapa, watu wetu wa Chadema wapo nyuma kabisa kule, embu nyoosheni mikono,” amesema Sugu huku wananchi wakiangua kicheko.

“Wamekuja huku wamewabana, na wewe unasema hutaki uvyama na mimi nimekushika na ninakufuata, katika watu wanaokuunga mkono bila kuhama vyama ni mimi.”

Sugu amemweleza Rais Magufuli kwamba, taarifa za kwamba sio kila kitu upinzani wanapinga na kuwa yapo baadhi ya mambo wanakubaliana naye.

Amesema, tatizo lililopo ni kuwa, yale ambayo wanakubaliana naye wasaidizi wake hawamwelezi isipokuwa, taarifa za kile wanachopingana naye ndio zimekuwa zikifikishwa kwake.

“Mr President (Mheshimiwa Rais) wasikwambie mambo haya eti tunakutusi, sijui hatukupendi, sio kweli,” amesema huku akimsifu kwa kutoa kauli kuwa, machinga wawe huru kufanya kazi zao.

Akisisitiza hilo Sugu amesema, mahali kokote duniani machinga huwa hawawekwi sehemu moja, “kuwekwa pamoja hii sio tabia yao kabisa.”

Amemwomba Rais Magufuli kupata ufumbuzi wa  kudumu wa upatikanaji maji Maji kutoka Mto Kiwira.

Amesema, kukamilisha mradi huo unaoihtaji Sh. 70 Bil kwa mujibu wa wataalamu, kutamfanya kuacha historia nzuri katika Jiji la Mbeya.

Pia Sugu amegusia msuguano uliopo kati ya wafanyabiashara wa Mbeya na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kwamba wamekuwa si rafiki wa wafanabiashara na kuomba wabadilike.

Hata hivyo, Sugu amemlalamikia Rais Magufuli kuwa, viongozi wa Mbeya wamemkamata mwenyekiti wake (hakumtaja jina) na kumweka ndani kwa madai ya kutaka kufanya vurugu.

“Jana kuna mwenyekiti wangu amekamatwa kwamba, anapanga amfanyie fujo rais, hakiwezekani hicho kitu na wewe umeona,” amesema Sugu na kuongeza;

“Haiwezekani watu na akili zao, wapange kumfanyia fujo rais. Nakuomba mimi ni kijana wako, niwe chanel (njia) ya dialogy (mazungumzo) ili kuondoa haya mafundofundo ya kisiasa kwa level ya Mbeya hata kitaifa ikiwezekana.”

Awali akimkaribisha Rais Magufuli Mbeya, Sugu alisema, mwaka jana kipindi kama hiki rais alipotembelea jiji hilo, yeye alikuwa gerezani.

“Mwaka jana kipindi kama hiki ulipokuja, mimi jamaa yako nilikuwa gerezani. Ukaja mpaka Iringa, nikasikia uko Iringa, nikawa nina wasiwasi kama utakuja Mbeya.

“Nikasema nitam ‘miss’ jamaa yangu, lakini nilivyosema nikasikia umeondoka na utarudi baadaye, nikasema Isha Allah akija tena atanikuta, na safari hii umekuja umenikuta niko nje. Mungu ni mwema sana.“

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!