Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM ‘amchana’ Sugu kiaina
Habari za Siasa

JPM ‘amchana’ Sugu kiaina

Dk. John Magufuli
Spread the love

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amesema, Jimbo la Mbeya Mjini halikuwa na msemaji na ndio maana alimteua Dk. Ackson Tulia kuwa ‘mbunge wake’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Amesema, wananchi wa Mbeya walimpa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, lakini jimbo hilo halikumpata msemaji, hivyo aliamua kumteua Dk. Tulia kuwa mbunge ili jimbo hilo lipate msemaji.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za urais katika Viwanja vya Airport ya zamani jijni humo leo tarehe 30 Septemba 2020, Dk. Magufuli amesema, kazi aliyofanya Dk. Tulia kwenye jimbo hilo, ilipaswa kufanywa na mbunge wa jimbo hilo.

Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ndio mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake.

Tulia amefanya kazi zote zilizotakiwa zifanywe na mbunge wa Mbeya. Leo nakushukuru sana (Dk. Tulia) kwa sababu ulinisumbua kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya.

“Na kwa vile sintakuteua tena kwa viti maalum, nimekuleta hapa kwa mama zako, dada zako, kaka zao wazee wako wakusulubu wewe kwa kazi nzuri ulizofanya,” Dk. Magufuli akimnadi Dk. Tulia ambaye ni mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM.   

Dk. Magufuli amewaambia wakazi wa jimbo hilo, kwamba mwaka 2015 wakati akigombea urais awamu ya kwanza, walimpa kura za kutosha lakini waligoma kumchagua mbunge aliyetokana na CCM.

“Mwaka 2015 tulipita hapa kuwaomba kura wana Mbeya, mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi sana hapa Mbeya, lakini kwa mbunge aliyekuwa wa CCM mkasema hapa.

“Mkanichagulia pia baadhi ya madiwani lakini mkanichagulia wabunge baadhi ya maeneo ya Mbeya…, hapa mjini mkasema hapana. Niseme kwa dhati nilisikitika lakini sikuwachukia,” amesema.

Hata hivyo amesema, alipota nya uchanguzi sababu za CCM kushindwa ubunge Mbeya Mjini, alibaini kuwepo kwa ugomvi nda ni ya wana CCM wenyewe.

Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ Mbunge wa Mbeya Mjini. Picha ndogo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson

“…na nikaja nikaambiwa, kushindwa kwa CCM katika jiji hili la Mbeya, ilitokana na ugomvi wa wana CCM wenyewe. Nilichofanya ndugu zangu, nataka niwaeleze hapa leo, katika kuhakikisha Mbeya haipotei kwenye ramani, nilimtafuta mwana mama mmoja msomi aliyekuwa akiitwa Dk. Tulia.

“Nikamteua kuwa mbunge kwamba yale yatakayokuwa yanajitokeza kwa ajili ya Mbeya, angalau yawe na msemaji. Nilpomteua kuwa mbunge, alipoingia bungeni akateuliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema.

Dk. Magufuli amewataka wakazi wa Mbeya kutofanya makosa tena kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kwamba “nileteeni Tulia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!