Rais John Magufuli

JPM amaliza utata wa JKT, Uyole na wananchi

RAIS John Magufuli amemaliza mvutano wa ardhi uliokuwepo kati ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wananchi na Kituo cha Utafiti wa Kilimo (Uyole) wilayani Nkasi, Rukwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

 Leo tarehe 8 Oktoba 2019, Rais Magufuli ameamua, katika ekari 27,000 zilizokuwa mikononi mwa JKT, Uyole wabaki na ekari 4,000 na ekari 1,000 ziende kwa wananchi.

Umuzi huo umetokana na malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Kalongwe kupitia diwani wao, kwamba hawana maeneo kwa ajili ya kilimo.

Kwenye ziara ya Rais Magufuli wilayani Nkasi, mkuu wa kikosi cha JKT wilayani humo amemweleza rais kwamba, awali kikosi hicho kilikuwa kikimiliki ekari 27,000 na baadaye kiliipa Uyole ekari 5,000.

“Siwezi kupunguza eneo la jeshi” amesema Rais Magufuli na kueleza kuwa, Uyole sasa wabaki na ekari 4,000 huku ekari 1,000 ziende kwa wananchi kwa ajili ya kilimo.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewapongeza JKT kwa kazi zao wanazozifanya na kwamba wanafanya vizuri kwenye maeneo ya mipaka huku akisisitiza “naomba mshirikiane nao.”

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Nkasi kulima kwa ili kuitendea haki ardhi waliyopewa kwa ajili ya shughuli hiyo “sasa naombeni mlime kweli,” amesema na kuongeza; “nitakuja kuuliza mmezalisha kiasi gani?”

RAIS John Magufuli amemaliza mvutano wa ardhi uliokuwepo kati ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wananchi na Kituo cha Utafiti wa Kilimo (Uyole) wilayani Nkasi, Rukwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).  Leo tarehe 8 Oktoba 2019, Rais Magufuli ameamua, katika ekari 27,000 zilizokuwa mikononi mwa JKT, Uyole wabaki na ekari 4,000 na ekari 1,000 ziende kwa wananchi. Umuzi huo umetokana na malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Kalongwe kupitia diwani wao, kwamba hawana maeneo kwa ajili ya kilimo. Kwenye ziara ya Rais Magufuli wilayani Nkasi, mkuu wa kikosi cha JKT wilayani humo amemweleza rais kwamba, awali kikosi hicho kilikuwa kikimiliki ekari…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram