Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM akerwa na mlundikano wa mahabusu, atoa agizo
Habari za Siasa

JPM akerwa na mlundikano wa mahabusu, atoa agizo

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amesema ni aibu nchi kuwa na idadi kubwa ya mahabusu, kuliko wafungwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 18 Desemba 2019, wakati akifungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita.

“Ni aibu kuwa na idadi kubwa ya mahabusu kuliko idadi ya wafungwa. Mnaweza mkaona changamoto tuliyonayo ya kupunguza mahabusu,” ameeleza Rais Magufuli.

Kufuatia changamoto hiyo, Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola kushirikiana na mahakama ili kuitatua changamoto hiyo.

Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyotoa haki kuimarisha mfumo wa utoaji haki ili kuharakisha uendeshaji wa mashtaka.

“Nitoe agizo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ofisi ya DPP, wakili mkuu wa serikali na polisi kushirikiana na mahakama ili kuimarisha mfumo wa haki na kuharakisha uendeshaji mashtaka nchini,” ameagiza Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!